Saturday , 18 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Green Acres kuwakatia bima wanafunzi wote
Elimu

Green Acres kuwakatia bima wanafunzi wote

Spread the love

Shule ya Green Acres imejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka 2023 / 2024 ikiwemo kuwakatia bima wanafunzi wa shule hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Pia imeahidi kujenga maabara, chumba cha compyuta, kuboresha na kuweka miundo mbinu yote kama madarasa, na vitendea kazi vyote kuwa bora kwa matumizi

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa shule ya msingi Green Acres, Minani Kafugugu wakati wa mahafali ya 23 ya shule ya awali, msingi na kidato cha nne yaliyofanyika shuleni hapo Mbezi Beach Salasala jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara, Taaluma, Utafiti na Ushauri, Dk. Nasib Mramba.

Alisema wamejipanga kuendelea kutoa taaluma bora na matokeo mazuri yenye tija kitaifa na kuwapa bima ya afya wanafunzi wote kidato cha kwanza hadi cha sita na kuongeza uhusiano wa shule na jamii yote majirani kiwilaya, mkoa na kitaifa

Naibu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dk. Nasibu Mramba akimpa cheti mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne shule ya Green Acres Mbezi Beach Salasala kwenye mahafali ya 23 yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkurugenzi wa shule za Green Acres Jackline Rushaigo

“Ubora wa elimu tuitoayo si katika taaluma tu, bali hata katika malezi na ustawi wa tabia, mwenendo wa afya kwa wanafunzi wetu hasa tukikumbuka kwamba tunaandaa taifa la kesho litakaloendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Ninaamini vijana wanaotoka Green Acres watakuwa mfano bora kwa wengine huko waendako,” alisema.

Alisema, ilikuwa na uhakika na ufuatiliaji wa maendeleo ya wanafunzi wake, shule  imeweka utaratibu wa wahitimu wote kukaa bweni na kwamba utaratibu huo umesaidia kwa walimu kumfikia mwanafunzi mmoja mmoja na kumsaidia kwa kadri ya mahitaji yake kitaaluma na kimalezi.

Alisema  tangu waanzishe utaratibu huo wamekuwa wakipata  matokeo mazuri sana kwa shule kufanya vizuri kwenye mitihani ya ndani ya mkoa na mitihani ya kitaifa kwa kushika nafasi za juu.

Aidha, alisema wameanzisha utaratibu wa kuabudu kwa itikadi zote yaani wakristo na waislamu ambapo  kila mwanafunzi na mfanyakazi anapata nafasi ya kuabudu kwa imani yake na pia wameanzisha masomo ya dini yaani Elimu ya dini ya Kiislam (EDK na Biblia).

Wahitimu wa darasa la saba wa wakiwa kwenye mahafali hayo mwishoni mwa wiki shuleni hapo Green Acres Mbezi Beach Salasala

Alisema shule ya Green Acres imekuwa ikifanya vema kitaaluma kwa mitihani mingi ya kitaifa kidato cha nne mwaka 2021 wanafunzi waliosajiliwa walikuwa 26 wa kike 15 wa kiume 11 shule haikuwa na Daraja 0 na wote waliendelea na elimu ya kidato cha 5 na wengine vyuo vya kati, mnamo mwaka jana 2022, wanafunzi walifaulu kwa daraja la I, II na III tu na hapakuwa na Daraja la nne wako 0 wote waliendelea na masomo katika ngazi mbalimbali kama kujiunga na kidato cha tano, Vyuo vya Afya, Biashara na ualimu

Alisema licha ya ushindani mkubwa uliopo kwa shule za binafsi,  shule hiyo imekuwa miongoni mwa shule zinazofanya vizuri katika utoaji wa elimu bora,  kutokana na msingi imara wa upendo na mshikamano uliojengwa na familia ya Green Acres pia mazingira bora na miundo mbinu

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Waziri SMZ akoshwa na kazi za Global Education Link

Spread the loveSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar SMZ imesema itaendesha msako na kuzifutia...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kufumua mitaala ya vyuo vikuu, ufundi stadi

Spread the loveSERIKALI inakusudia kufanya mapitio katika mitaala na programu za vyuo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

error: Content is protected !!