Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Kagame kuwania muhula wa nne
Kimataifa

Rais Kagame kuwania muhula wa nne

Rais wa Rwanda Paul Kagame
Spread the love

Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema atawania muhula wa nne katika uchaguzi wa rais mwaka ujao. Anaripoti Matilda Peter kwa msaada wa Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

“Ndiyo, hakika mimi ni mgombea,”Kagame aliambia jarida la lugha ya Kifaransa la Jeune Afrique jana Jumanne.

Alipoulizwa kuhusu nchi za Magharibi zitachukulia vipi uamuzi wake wa kugombea tena, Kagame alisema, “Samahani kwa nchi za Magharibi, lakini kile ambacho nchi za Magharibi hufikiri si tatizo langu”.

“Nimefurahishwa na imani ambayo Wanyarwanda wanayo kwangu. Nitawatumikia daima, kadri niwezavyo,” aliongeza Kagame

Kagame alitania mwezi Aprili kwamba anatazamia kustaafu na kukabidhi madaraka baada ya miaka 23 madarakani.

Chama tawala nchini humo, Rwandan Patriotic Front (RPF-Inkotanyi), kilimuacha Kagame kuendelea kuhudumu kama mwenyekiti wake mwezi Aprili. Ameongoza chama hicho tangu 1998.

Kagame amekuwa rais wa taifa hilo la Afrika Mashariki tangu mwaka wa 2000. Kura ya maoni iliyozua utata mwaka 2015 iliondoa ukomo wa mihula miwili ya kikatiba kwa marais.

Alishinda uchaguzi uliopita wa 2017 kwa asilimia 98.8 ya kura.

Rwanda chini ya Rais Kagame imekuwa na utulivu wa kisiasa lakini wakosoaji na makundi ya haki za binadamu yanaituhumu serikali yake kwa kuweka mipaka ya uhuru wa kisiasa na kukandamiza upinzani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!