Monday , 13 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Trump kujisalimisha kesi ya kubatilisha uchaguzi
Kimataifa

Trump kujisalimisha kesi ya kubatilisha uchaguzi

Donald Trump
Spread the love

RAIS wa zamani wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa atajisalimisha mwenyewe jimboni Georgia Alhamis wiki hii ili kukabiliana na mashtaka ya udanganyifu na makosa yanayohusu tuhuma za kutaka kubatilisha matokeo ya uchaguzi. Anaripoti Maryam Mudhihir kwa msaada wa mitandao ya kimataifa…(endelea.)

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social siku ya jana Jumatatu, Trump alisema kwamba siku hiyo ya Alhamis atakamatwa na Mwanasheria mwenye misimamo mikali, Fani Wills, ambaye alifungua mashtaka ya manne mwaka huu dhidi yake.

Jaji katika kesi hiyo, awali aliidhinisha dhamana ya Dola za Kimarekani 200,000 kwa Trump katika kesi hiyo ya udanganyifu iliyofunguliwa dhidi yake katika jimboh hilo la kusini.

Trump na washitakiwa wengine 18 katika kesi hiyo ya kihistoria watakuwa na muda wa mwisho wa hadi saa sita mchana siku ya Ijumaa kujisalimisha wenyewe katika mamlaka za Georgia.

Kwenye ujumbe wake kupitia Truth Social, Trump amedai kwamba mwanasheria Wills anashirikiana na wizara ya sheria ‘kihuni’.

Trump anadai kuwa mashtaka yote dhidi yake yamesukwa ili kuzuia jaribio lake la kuwania muhula wa pili wa urais wakati akiongoza ndani ya chama chake cha Republican.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

error: Content is protected !!