Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwabukusi, Mdude nao waachiwa kwa dhamana
Habari za SiasaTangulizi

Mwabukusi, Mdude nao waachiwa kwa dhamana

Spread the love

 

HATIMAYE Wakili, Boniphace Mwabukusi na Kada wa Chasema, Mpaluka Saidi Nyangali maarufu kama ‘Mdude’ nao wameachiwa huru na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya baada ya kutimiza masharti ya dhamana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Wawili hao wameachiwa huru jioni leo Ijumaa ikiwa ni saa chache baada ya Dk. Willibroad Slaa naye kuachiwa huru mchana na Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Wakili wa wawili hao, Philip Mwakilima amesema watuhumiwa hao awali waliandikishwa maelezo kuwa watuhumiwa wa makosa ya uhaini lakini sasa wameachiwa kwa tuhuma za uchochezi.

“Leo asubuhi tulipewa taarifa kwamba tuwajulishe ndugu wa wateja wetu walete wadhamini na sasa wamedhaminiwa wakituhumiwa na kosa la uchochezi. Kila mtuhumiwa alitakiwa awe na wadhamini wawili wawe na mali isiyohamishika yenye thamani isiyo chini ya Sh 10 milioni pamoja na barua kutoka serikali za mitaa,” amesema.

Naye Wakili Mwabukusi akizungumza baada ya kuachiwa huru mbali na kushukuru Watanzania amesema Mungu amewatumia kama sauti ili wawe nje leo kwani lengo la mashtaka hayo ya uhaini ni kuwaua kama ilivyo adhabu yake.

 

“Kwa hiyo walitaka tunyongwe kwani ndio adhabu ya shtaka hilo. Tunaamini Mungu amewatumia kupaza sauti tunawashukuru sana, tuwahakikishie tutatoa maelezo yetu na muelekeo wetu,” amesema na kuongeza;

“Ila watambue kwamba hatujayumbishwa hatujatetereshwa wala kubabaishwa katika kutimiza wajibu wetu kama watanzania, naamini ndege ikipaa huwa haina reverse, kwa hiyo msimamo upo palepale kama tulivyomaliza hatua yetu ya mwisho.”

Amesema licha ya kwamba wameachiwa, ni kwamba walikuwa kizuizini jambo ambalo ni kinyume cha katiba.

“Niko hapa kwa sababu ya solidarity ya ndani na nje ya nchi, na vyombo vya habari… ninawashukuru sana ila kwa leo kwa sababu nina complication kidogo za afya, mwili haupo stable sana nitasema bayana what next,” amesema.

Kwa upande wake Mdude amesema baada ya kutoka kizuizini walipokuwa wamewekwa kwa siku tisa, watawasiliana na mwenzao Dk Slaa ili waanzie walipoishia.

“Tunaanzia tulipoishia ngoma hairudi nyuma. Tutazungumza na waandishi wa habari kwamba tutaendaje mbele kwani haturudi. Maandamano sio kosa la uhaini halijakatazwa na sheria yoyote ya nchi… mkiniweka humo ndani mnanitekenya, polisi ni sebule, gerezani ni chumbani kwangu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!