Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Slaa amuomba mambo 3 Rais Samia “toa kauli utuokoe”
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa amuomba mambo 3 Rais Samia “toa kauli utuokoe”

Rais Samia na Dk. Slaa
Spread the love

BALOZI Mstaafu Dk. Wilbroad Slaa amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan atokeo hadharani atoke hadharani na kutoa kauli ili kuliokoa Taifa katika janga lililoibuka kwenye mkanganyiko wa mkataba wa uwekezaji kwenye bandari ya Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Dk. Slaa amesema Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alisaini mkataba huo kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kupitia kampuni ya DP World kwa kibali cha Rais Samia na mamlaka yake ambayo yameliingiza Taifa katika msiba mkubwa.

Akizungumza leo katika mkutano ulioandaliwa na Chadema kwa kushirikiana na Sauti ya Watanzania anayoongoza, Dk. Slaa amesema anaomba hivyo kwa sababu nchi ipo kwenye kilio.

“Hili la bandari mama nakuomba wewe ndiye uliyeshuhudia uwekaji saini wa Mkataba wa makubaliano (MOU) kati ya TPA na DP World hajawahi kutokea Rais anashuhudia tukio la aina hiyo.,

‘Pili nakuomba wewe uliweka saini power off attorney ukimruhusu Mbarawa asaini mikataba kati ya Tanzania na Dubai. Mbarawa alifanya kwa kibali chako kwa mamlaka yako umeingiza Taifa katika msiba mkubwa, toka hadharani kwa kauli… Rais Tanzania hakuna mwingine ni wewe toka utuokoe katika janga hili.

“Mwisho tumeingia kwenye haya kwa sababu ya katiba mbovu, kama isingekuwa mbovu wabunge kule Dodoma wasingefanya kiini macho walichofanya tarehe 10,” amesema Dk. Slaa.

Aidha, Dk. Slaa amemuomba Rais Samia kuwaandalia mazingira ya upatikanaji wa Katiba mpya na si kuwaandalia Katiba mpya kwani katiba hiyo ikipatikana ataongoza Taifa vizuri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yatoa kauli wanaolala nje Hospitali ya Muhimbili

Spread the loveSERIKALI imesema inajipanga kushirikiana na sekta binafsi kujenga majengo yatakayosaidia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Migogoro ya ndoa yaongezeka, Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveMIGOGORO ya ndoa na familia imeongezeka kwa asilimia 8.3  kutoka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

error: Content is protected !!