Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Tulia atoa maagizo serikalini ajira za watumishi wanaojitolea
Habari za Siasa

Spika Tulia atoa maagizo serikalini ajira za watumishi wanaojitolea

Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson
Spread the love

 

SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, ameagiza Serikali kuweka kanzi data maalum (data base), yenye taarifa za watumishi wanaojitolea ili wapewe kipaumbele katika mchakato wa ajira. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Spika Tulia ametoa agizo hilo leo tarehe 6 Aprili 2023, bungeni jijini Dodoma, baada ya Mbunge Viti Maalum, Felista Njau kuhoji lini Serikali itaajiri watalaamu wanaojitolea kwa muda mrefu kufanya kazi katika sehemu mbalimbali nchini.

“Waziri wa Afya na wa TAMISEMI, nafikiri kuna haja ya kukaa na Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, sababu watumishi wa afya wanaojitolea na walimu wanaojitolea huwa haipendezi sana kuachwa kwenye ajira. Sababu ajira zikitangazwa wale wanaojitolea unajikuta kwenye eneo lako hakuna mmoja aliyepata ajira, tunajiuliza hawana sifa na wanaokaa nyumbani ndiyo wana sifa?” amesema Dk. Tulia na kuongeza:

“Nafikiri mtengeneze utaratibu mzuri ili kila mwaka mpate taarifa za wanaojitolea ili ajira zinapopatikana mzitumie taarifa hizo kuwapa kipaumbele.”

Awali akimjibu Njau, Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, alisema wizara imetoa muongozo wa kuwalipa nusu mshahara watumishi wanaojitolea kwa kutumia mapato ya ndani.

Aidha, Dk. Mollel alisema hospitali za mikoa, kanda na taifa zimeweza kuwalipa mishahara kamili asilimia 40 ya watumishi wanaojitolea , kwa kutumia mapato ya ndani.

Alisema Wizara ya Afya, itashirikiana na Wizara Ofisi ya Rais TAMISEMI, kuangalia namna bora ya kuwapa kipaumbele kwenye ajira watumishi wanaojitolea kuliko waliokuwa nje ya mfumo huo wakisubiri ajira moja kwa moja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!