Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Spika Tulia awapa neno mawaziri utekelezaji mashamba ya pamoja
Habari Mchanganyiko

Spika Tulia awapa neno mawaziri utekelezaji mashamba ya pamoja

Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson
Spread the love

 

SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewataka mawaziri kushirikiana kwa pamoja katika utekelezaji wa mashamba makubwa ya pamoja katika Programu ya Building Better Tomorrow (BBT), ili yaongezeke kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa chakula nchini na ajira kwa vijana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Spika Tulia ametoa wito huo leo tarehe 20 Machi 2023, katika uzinduzi wa mashamba hayo uliofanyika jijini Dodoma.

“Mashamba haya ya mfano tunaamini yataendelea kuwa mengi zaidi, yanahitaji ushirikiano wa wizara zote. Mashamba haya yanahitaji kumwagiliwa yanahitaji pampu na pampu zinatumia umeme kwa hivyo waziri wa nishati sisi kama Bunge tunatamani kuona anaeleza vipi ili jambo hili liweze kuwa na uhalisia,” amesema Spika Tulia.

Spika Tulia amesema “hapa yuko waziri wa uwekezaji tunazungumza kuhusu kuilisha Tanzania na dunia, lakini tunahitaji viwanda ili biashara yetu ikue zaidi, tunahitaji uwekezaji zaidi. Naomba sana wizara zako zote na naamini katika bajeti ijayo hiki ulichokizindua leo tutaona muunganiko wa Serikali ikiwa moja kwenye hili suala la mapinduzi ya kilimo.”

Aidha, Spika Tulia amesema Bunge litaendelea kumuunga mkono Rais Samia katika utekelezaji wa program hiyo.

Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Sophia Mjema, amempongeza Rais Samia kwa kuanzisha mradi huo huku akiahidi chama chake kitaendelea kuunga mkono katika utekelezaji wa mikakati yake atakayoipanga.

“Leo tunashuhudia mashamba makubwa watakayokuwa wanapata vijana, Serikali yako itakuwa inaendelea kutoa ajira, kunyanyua uchumi wa Tanzania lakini muhimu kuwa na uhakika wa chakula katika nchi yetu na jirani, sina shaka Tanzania itakuwa ghala la chakula,” amesema Dk. Mjema na kuongeza:

“Sababu mama unajali familia na unataka kuona watoto wasife njaa, CCM kinakupongeza na kuridhishwa na utekelezaji ilani ambayo unasimamia na Serikali yako, tutakuunga mkono na tuko nyuma yako kuhakikisha yale unayopanga kwenye mikakati yatakwenda kufanyika.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

error: Content is protected !!