Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Xi Jinping awasili Urusi, kufanya mazungumzo na Putin
Kimataifa

Xi Jinping awasili Urusi, kufanya mazungumzo na Putin

Rais wa China Xi Jinping
Spread the love

 

RAIS wa uchini Xi Jinping amewasili sasa nchini Urusi, na kulingana na Shirika la habari la Urusi TASS news , Xi Jinping amewasili katika uwanja wa ndege wa Vnukovo muda mfupi uliopita.

Anatarajiwa kula chakula cha mchana pamoja na mwenyeji wake Rais wa Urusi Vladimir Putin kabla ya kufanya mazungumzo ya ana kwa ana.

Je viongozi hawa wawili wanatarajiwa kuwa na mazungumzo gani?

Chini ya mwezi mmoja uliopita, China ilipendekeza vipengele 12 , vya mpango wa amani katika jaribio la kutatua mzozo wa vita nchini Ukraine, ikatoa wito wa mazungumzo ya amani na kuheshimu mamlaka ya taifa.

Lakini waraka haukuzungumzia kwamba Urusi lazima iondoe majeshi yake nchini Ukraine, na pia ulilaani matumizi ya “vikwazo vya jumla” katika kile ambacho kinaonekana kama ukosoaji uliofunikwa kwa mataifa washirika wa ukraine katika Magharibi.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin

Muda mfupi baada ya kufichuliwa kwa mpango huo, Urusi ilisifu mapendekezo hayo ya amani ya China. Na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema anatumai China haitatoa silaha kwa Urusi.

Mshauri wa ngazi ya juu wa rais wa Ukraine, Mykhaylo Podolyak, aliviambia vyombo vya habari vya Italia kuwa kuna “utata kabisa” kati ya usisitizwaji wa mpango kuhusu kuheshimiwa kwa utaifa na uadilifu wa eneo kwa ajili ya usitishaji wa mapigano – ambako Podolyak anauzungumzia utakaoiacha Urusi ikidhibiti maeneo iliyo yatwaa.

Akizungumza kabla ya mazungumzo ya leo kati ya Xi na Putin , msemaji wa ofisi ya Rais, Dmitry Peskov alisema wawili hao watajadili mada zilizopendekezwa na Beijing katika mpango wa amani kwa ajili ya Ukraine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!