Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Maandamano Kenya, Afrika Kusini yashika kasi, wapinzani wakishikiliwa
Kimataifa

Maandamano Kenya, Afrika Kusini yashika kasi, wapinzani wakishikiliwa

Spread the love

 

MAANDAMANO ya kupinga serikali zilizoko madarakani nchini Kenya na Afrika Kusini, yameendelea kushika kasi katika mataifa hayo, huku baadhi ya walioandamana wakitiwa nguvuni na Jeshi la Polisi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Maandamano nchini Kenya yaliitishwa na aliyekuwa Mgombea Urais wa Kenya kupitia Chama cha Azimio la Umoja, Raila Odinga, huku ya nchini Afrika Kusini, yakiitishwa na chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters, ambayo yanafanyika leo Jumatatu,tarehe 20 Machi 2023.

Huko nchini Kenya, Jeshi la Polisi linajaribu kuyazuia maandamano yanayofanyika jijini Nairobi ambapo waandamanaji wanalenga kutinga Ikulu ya taifa hilo, ambapo hadi sasa wabunge wa upinzani, Amina Mnyazi na Ken Chonga, pamoja na seneta wa Kilifi, Stewart Madzayo, wamekamatwa.

Pia, aliyekuwa Spika wa Kaunti ya Nakuru na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha ODM, katika kaunti hiyo, Joel Kairu, amekamatwa na Jeshi la Polisi.

Licha ya wapinzani hao kukamatwa, Azimio la Umoja kupitia akaunti yake ya Twitter, umeandika ukisema hautarudi nyuma katika maandamano hayo.

Wakati wabunge hao wa Kenya wakitiwa nguvuni, nchini Afrika Kusini watu takribani 100 walioshiriki maandamano wameripotiwa kukamatwa na Jeshi la Polisi kwa madai kwamba wamefanya maandamano ya fujo.

Waziri wa Polisi nchini humo, Bheki Cele, ametoa taarifa akisema asilimia kubwa ya waliokamatwa wanatoka Jimbo la Gauteng.

Cele amedai kuwa, waliokamatwa walikuwa wakitengeneza vilipuzi vya moto, kufunga barabara na kujaribu kuwazuia watu kwenda kazini.

Maandamano hayo ya nchini Afrika Kusini,yanalenga kumshinikiza Rais wa taifa hilo, Cyril Ramaphosa ajiuzulu kwa madai kuwa ameshindwa kutekeleza majukumu yake katika kuimarisha uchumi, kuongeza ajira na kupunguza makali ya ugumu wa maisha.

Nako nchini Kenya, maandamano yanalenga kumshinikiza Rais William Ruto, ajiuzulu kwa madai kwamba ameshindwa kudhibiti mfumuko wa bei.

8 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

error: Content is protected !!