Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wawili kizimbani kwa kukwepa kodi ya bilioni 6.
Habari Mchanganyiko

Wawili kizimbani kwa kukwepa kodi ya bilioni 6.

Spread the love

 

WANANDUGU wawili, Sibtain Murji 43 na Zameen Murji 47 wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kukwepa kodi kiasi cha Sh. Bilioni sita. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Sylivia Mitanto akisaidiana na wakili Emmanuel Medalakini imedai kuwa tarehe isiyojulikana kati ya Januari 2021 Desemba 2022 jijini Dar es Salaam washtakiwa walishindwa kupeleka tamko la Mapato la biashara iliyosajiliwa kwa jina la Murji Brothers na kupelekea kukwepa kodi ya Sh. 6,224,341983.09/=

Pia inadaiwa, siku na mahali hapo washtakiwa hao kwa pamoja kwa makusudi, walikwepa kodi kwa njia ya udanganyifu na kuisababishia TRA hasara ya kiasi cha fedha zaidi ya Sh. 6 bilioni.


Katika shtaka la utakatishaji fedha inadaiwa, Sikh na mahali hapo washtakiwa hao walijipatia kiasi hicho cha fedha cha sh. bln 6/- huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kukwepa kodi.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 3 Machi, 2023.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yapata tuzo ya mwezeshaji bora wa mikopo serikali Afrika

Spread the loveBenki ya NBC imepata tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Pamoja...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!