Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbatia, wenzake wakwaa kigingi, Mahakama yawatambua wajumbe wapya wa bodi
Habari za Siasa

Mbatia, wenzake wakwaa kigingi, Mahakama yawatambua wajumbe wapya wa bodi

Joseph Selasini (kulia) na James Mbatia
Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imetoa uamuzi wa kuwatambua wajumbe wapya wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha NCCR-Mageuzi, hadi kesi ya msingi iliyofunguliwa na wajumbe wa zamani kupinga uhalali wa vikao vilivyowateua itakapotolewa uamuzi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Uamuzi huo umetolewa na mahakama hiyo jana tarehe 6 Februari 2023, mbele ya Jaji Ephery Kisanya, wakati kesi hiyo ndogo Na. 570/2023, ilipokuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Jaji Kisanya alitoa uamuzi huo akisema, kama mahakama hiyo ingetoa uamuzi kuhusu uhalali wa vikao vilivyofanya uteuzi wao, ingeathiri kesi ya msingi ambayo bado haijatolewa uamuzi.

Amesema kuwa, mahakama hiyo imeamua kuwatambua wajumbe hao ambao ni Beati Mpitabakama, Ester Komba, Laila Rajab Hamis, Mtumwa Ame Hamis na Idrisa Omary Haji, kulingana na ushahidi ulioletwa mahakamani hapo na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), uliowatambua kuwa ni wajumbe halali.

Kesi hiyo ndogo ilifunguliwa na wajumbe wa zamani, Mohamed Tibanyendera na wenzake, dhidi ya Joseph Selasini na wenzake, wakiwatuhumu kuwaondoa katika nyadhifa zao kinyume cha sheria, kisha kujiteua katika nafasi hizo.

Katika kesi hiyo, Tibanyendera na wenzake walidai kikao kilichotumika kuwaondoa ujumbe tarehe 23 Mei 2022 hakikuwa halali.

Baada ya mahakama kutoa uamuzi huo, Jaji Kisanya ameahirisha kesi ya msingi hadi tarehe 14 February 2023, itakapokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Katika kesi ya msingi Na. 150/2022, Tibanyendera na wenzake wanapinga kufukuzwa NCCR-Mageuzi wakidai kwamba mkutano uliotoa maamuzi hayo tarehe 21 Mei 2022 haukuwa halali kwa kuwa uliahirishwa na uongozi wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wake anayedaiwa kufukuzwa, James Mbatia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!