Idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko lililotokea jana Jumatatu katika mpaka wa Syria na Uturuki, imeongezeka hadi kufikia zaidi ya 4,800 bada ya waokozi kuendelea na zoezi hilo usiku kucha. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Waokozi hao wanawatafuta watu walio chini ya kifusi baada ya tetemeko hilo la ardhi ambapo hadi sasa Uturuki imethibitisha vifo 2,379 huku Syria ikirekodi vifo zaidi ya 1,400.
Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa yamkini waliokufa ni mara nane zaidi ya idadi inayojulikana hivi sasa.
Wizara ya Afya ya Uturuki imesema kuwa magari ya kubeba wagonjwa yapatayo 813 yamepelekwa katika maeneo yaliyoathirika, na vikundi maalumu vya huduma za dharura zaidi ya 220 vimeambatana na magari hayo.
Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.8 kwenye kipimo cha Richter liliitikisa sehemu ya katikati mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria alfajiri ya jana, na kufuatiwa na jingine dakika 10 baadaye, likiharibu vibaya miundombinu katika miji ipatayo 12.
Leave a comment