Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia aipa miezi minne tume kupitia mfumo haki jinai
Habari za Siasa

Rais Samia aipa miezi minne tume kupitia mfumo haki jinai

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, ameitaka tume aliyoiunda kuangalia jinsi ya kuboresha taasisi za haki jinai nchini, kukamilisha kazi hiyo ndani ya miezi minne, ili ripoti yake ipatikane mwishoni mwa Mei, 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Jumanne, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, wakati anaizindua tume hiyo.

“Muda ambao tuliupanga mwanzo wa miezi mitatu lakini kutokana na ukubwa wa kazi na hadidu rejea mlivyozitizama mkasema hapana tunaomba miezi minne. Kwa hiyo sisi tumekubali miezi minne mtafanya kuanzia kesho hadi tarehe 30 Mei 2023 tutapata ripoti kamili au ya kwanza, inategemea muda utakavyokuwa,” amesema Rais Samia.

Mkuu huyo wa nchi amesema kuwa, mfumo wa haki jinai nchini umevurugika kutokana na tasisi zinazousimamia kukiuka maadili yake.

“Tunakubaliana kwamba katika kipindi cha miongo kadhaa mfumo wa haki jinai nchini umevurugika kwa sababu nadhani ya kupuuza na sio kutokuwa na mkifumo ya maadili, sababu katika kila taasisi zina mfumo wake wa kazi lakini kuendana na ile mifumo ya maadili ndiyo imekuwa tatizo, kutokana na hayo kupotea kwa haki za watu hasa wasio uwezo, mamlaka wala fedha wamekuwa wakipoteza sana,” amesema Rais Samia.

Rais Samia ameitaka tume hiyo kufuatilia utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ili kubaini kama inatekeleza wajibu wake au inahamasisha kukua kwa vitendo hivyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!