Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bashiru aibuka na bei za vyakula, “Njaa inadhalilisha nchi”
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Bashiru aibuka na bei za vyakula, “Njaa inadhalilisha nchi”

Bashiru Ally
Spread the love

MBUNGE wa kuteuliwa na Rais, Dk. Bashiru Ally, ameitaka Serikali kuja na mikakati ya kutatua changamoto ya mfumuko wa bei za vyakula huku akisema kwamba njaa inadhalilisha  heshima ya uhuru wa nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Dk. Bashiru ameyahoji hayo leo tarehe 31 Januari 2023, bungeni jijini Dodoma.

“Njaa inadhalilisha heshima ya uhuru wa nchi, njaa inatweza utu wa binadamu. Kwa hiyo tatizo la mfumuko wa bei za vyakula ni tatizo ambalo tutake tusitake lazima tuongeze kiwango cha ubunifu kukabiliana nalo,” amesema Dk. Bashiru.

Mbunge huyo amedai kuwa, kuna baadhi ya wananchi wameanzisha utaratibu wa kupata milo miwili kwa siku badala ya mitatu kama ilivyozoeleka ili kumudu gharama za vyakula.

“Nilikuwa nazungumza na baadhi yao mmoja anasema wamepanga milo kwa kupiga pasi kwa maana kwamba asubuhi na chakula cha mchana vinaunganishwa kwenye majira ya saa 5 na 6 asubuhi, halafu mlo wa usiku unaunganishwa kati ya saa 11 na 12 jioni, hawasubiri kujadili mambo ya Ukraine na tabia ya nchi,” amesema Dk. Bashiru.

Dk. Bashiru amesema “kama wameanza kuchukua hatua  wananchi wanakabiliana na hali hiyo nchi ianenda maendeleo yanaendelea hatujasimama, kwa nini Serikali isipanue wigo wa kufikiri na ubunifu kukabiliana na njaa?”

Katika hatua nyingine, Dk. Bashiru amehoji jitihada za Serikali katika kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa hususan vyakula, zimezaa matunda gani, huku akihoji kwa nini haidhibiti uuzaji holela wa mazao ya vyakula nje ya nchi.

“Nimalize kwa kuacha maswali machache, je ruzuku ya mbolea , mafuta na mbegu umepunguza ukali kiasi gani ya mfumuko wa bei ya vyakula. Je, kutokuwa na karantini kumepunguza kiasi gani makali ya mfumuko wa bei za vyakula. Je, udhibiti wa kuuza vyakula nje ukiwepo unamnufaisha nani na pia vyakula vikiuzwa nje kwa uwazi hiyo ruksa inamnufaisha nani?” amehoji Dk. Bashiru.

Aidha, Dk. Bashiru ameishauri Serikali kuwatengezea mazingira bora ya uzalishaji wakulima, wavuvi na wafugaji ili wazalishe chakula kwa wingi kwa ajili ya kudhibiti mfumuko huo.

Akielezea athari zinazowakabili wananchi kutokana na mfumuko huo, Dk. Bashiru amedai baadhi yao wanapata mlo mara mbili kwa siku kutokana na kushindwa kumudu gharama za vyakula kutokana na kipato chao kuwa kidogo.

1 Comment

  • Serikali inatoa ruzuku katika mbolea, mbegu na mafuta izi kupunguza gharama kwa wakulima. Halafu mazo yao wanayauza nje ya nchi
    Fedha zetu za tozo na kodi zinasaidia nchi za jirani wakati wananchi wetu wanaishi na njaa. HUU NI WIZI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!