Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yafufua mradi wa maji uliotelekezwa miaka 60 iliyopita
Habari Mchanganyiko

Serikali yafufua mradi wa maji uliotelekezwa miaka 60 iliyopita

Spread the love

ZAIDI ya wananchi elfu tano wa Kijiji cha Msimba wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji safi na salama baada ya serikali kutumia  shilingi milioni 400  kukamilisha kuufufua mradi  wa maji uliotelekezwa na wajerumani miaka zaidi ya 60 iliyopita. Anaripoti Christina Haule, Kilosa … (endelea).  

Akitoa taarifa ya mradi huo,mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira MORUWASA  Mhandisi Tamimu Katakweba alisema awali wananchi hao walikuwa wakitumia hayo jana mbele ya Waziri wa maji  Jumaa Aweso alipotembelea na kuzindua mradi huo.

Katakweba alisema wakazi hao walilazimika kutumia maji ya visima na mito kutokana na kukosa huduma ya uhakika ya maji safi na salama.

Alisema juhudi za kusogeza maji kwa wananchi ni safari ya kufikia malengo ya asilimia 85 ya upatikanaji wa maji Vijijini ikizidi kushika kasi na kutatua changamoto ya maji kwa wananchi.

 

Mkurugenzi wa MORUWASA alisema hiyo ni hatua nzuri ya mafanikio kama wataalamu kwa kuona sasa wananchi wanaaza kunufaika na miradi ya maji ukiwemo mradi huo utakaohudumia wakazi wa vijiji mbalimbali ikiwemo vya Mikumi na Msimba.

Naye Waziri wa maji Jumaa Aweso aliwaagiza wananchi wa vijiji hivyo kutunza vyanzo na miundombinu ya  miradi ya maji  uliotelekezwa  hapa na serikali ya kikoloni miaka zaidi ya sitini iliyopita ambapo sasa serikali imeufufua kwa lengo la kuendeleza dhamira ya kumtua mama ndoo kichwani.

Nao wananchi wa kijiji cha Msimba waliishukuru Serikali kwa jitihada zake za kuhakikisha wanapata maji safi waliyoyakosa kwa miaka mingi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA wawanoa mama lishe 50 kukabiliana na majanga ya moto

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

error: Content is protected !!