Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Afungwa miaka 30 jela kwa kumbaka dada’ke
Habari Mchanganyiko

Afungwa miaka 30 jela kwa kumbaka dada’ke

Spread the love

 

MKULIMA Frank Kigomba, amehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Kilolo,mkoani Iringa, kifungo cha miaka 30 jela pamoja na kulipa fidia ya Sh. 500,000, kwa kosa la kumbaka dada yake wa kuzaliwa ili apate utajiri. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi leo Jumamosi, kupitia ukurasa wake wa Twitter, Kigomba amepewa adhabu hiyo tarehe 5 Januari 2023 na hakimu wa mahakama hiyo, Tumaini Maleko.

“Mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani kwa kosa hilo ambapo alisomewa shtaka la kumbaka dada yake wa kuzaliwa tarehe 2 Januari 2023 ndani ya nyumba anayojenga kutokana na imani za kishirikina za kutaka kuwa tajiri baada ya kudanganywa na mganga kuwa akifanya hivyo atakuwa tajiri,” imesema taarifa ya Jeshi la Polisi na kuongeza:

“Baada ya mtuhumiwa kusomewa shtaka lake mahakamani hapo alikiri kosa na hivyo kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela sambamba na kumlipa dada yake fidia ya kiasi hicho cha fedha Sh. 500,000.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA wawanoa mama lishe 50 kukabiliana na majanga ya moto

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

error: Content is protected !!