Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Sakatala la kodi: TRA yamuita Dimond Platnumz
Habari Mchanganyiko

Sakatala la kodi: TRA yamuita Dimond Platnumz

Spread the love

BAADA  msanii na mfanyabiashara Nasibu Abdul (Diamond Platnumz), kutoa malalamiko dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwamba ina lengo la kuiua  Kampuni ya Wasafi Media, anayoimiliki, mamlaka hiyo imemuita kwa ajili ya mazungumzo zaidi.Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

TRA imetoa taarifa ya wito huo jana usiku tarehe 30 Desemba 2022, baada ya Dimond Platnumz kupitia kituo cha redio cha Wasafi Fm, kudai kwamba maafisa wa TRA walivamia kwa nguvu katika ofisi za chombo hicho cha habari, pamoja na kuchukua kiasi cha fedha katika akaunti zake kimabavu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi ya TRA, malalamiko ya msanii huyo yanahusu ukiukwaji wa sheria za kodi na kwamba mamlaka hiyo haiwezi kutoa maelezo kwa undani kwa umma, kutokana na katazo la kisheria linaloilazimu kutunza siri za walipakodi.

Hivyo, TRA imefanya mawasiliano na Diamond Platnumz kwa ajili ya mazungumzo na maelekzo zaidi.

“Suala analolilalamikia Nasibu Abdul linahusu ukiukwaji wa sheria za kodi, hata hivyo sheria hairuhusu kutolea maelezo kwa undani kutokana na katazo la kisheria linalotulazimu kutunza siri za walipakodi. Pamoja na maelezo haya mawasiliano yamefanyika na mhusika kwa njia ya barua ya wito kwa mazungumzo na maelekezo zaidi,” imesema taarifa ya TRA.

Akifunguka zaidi kuhusu sakata hilo, Dimond alidai TRA ina bomoa uwekezaji wake pamoja na kufanya unyanyasaji kwa kuwa kama kulikuwa na tatizo lolote alikuwa tayari kutoa ushirikiano badala ya mamlaka hiyo kuchukua uamuzi wa kuvamia ofisi yake.

“Sisi tuko vizuri kwenye masuala ya kodi na kila kitu, kama kuna sehemu ya kutuelekeza tuelekezeni kama walezi wa sekta hii lakini msifanye kutubomoa sababu jana nimesikia TRA wamevamia Wasafi Media, kitendo hicho ni kama unyanyasaji,” alidai Diamond na kuongeza:

“Kwanza mkurugenzi mwenyewe ukinipigia simu dakika moja nitafika, lakini kutufanyia hivyo ni kama kutunyanyasa katika nchi yetu na kupandikiza chuki tuone kama serikali inatukandamiza.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile aukwaa uenyekiti wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!