Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yaongoza tuzo za mwajiri bora, yafikisha 22
Habari Mchanganyiko

NMB yaongoza tuzo za mwajiri bora, yafikisha 22

Spread the love

BENKI ya NMB imetangazwa kuwa Mwajiri bora wa mwaka 2022 katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) jijini Dar es Salaam mwishoni. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Benki hiyo mbali na kushinda Tuzo ya mshindi wa jumla kama Mwajiri Bora wa Mwaka pia ilinyakua tuzo nyingine mbili za kampuni bora kwenye mashirika makubwa na tuzo ya Kampuni Bora kwenye Sekta Binafsi na kufanya jumla ya tuzo ilizoshinda benki hiyo kufikia 21 hadi sasa kwa mwaka 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango (kulia) akimkabidhi Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay (katikati), Tuzo ya Mwajiri Bora 2022 baada ya NMB kuibuka mshindi wa jumla katika hafla ya utoaji tuzo hizo zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hizo, Afisa Mkuu Rasilimali Watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay alisema kutajwa kuwa mwajiri namba moja nchini kunathibitisha nafasi ya benki hiyo kuwa mwajiri bora zaidi katika soko la Tanzania.

“Tunafurahi leo tumetunukiwa tuzo ya Mwajiri Bora wa ujumla baada ya kushinda tuzo nyingi mwaka huu. Maono yetu ni kuwa taasisi inayoongoza katika kusaidia kujenga mustakabali mwema kwa Watanzania wote.

“Kama sehemu ya mkakati wetu wa biashara, tunawekeza pakubwa katika kujenga utamaduni jumuishi ambapo wafanyakazi wetu wanathaminiwa  na kushirikishwa katika mabo yanayohusu biahsra na maslahi yao,” alisema Akonaay

Akonaay alisema benki yake inatoa kipaumbele kwa wafanyakazi wake na kutilia mkazo katika kujenga na kuendeleza uwezo wa viongozi sehemu za kazi kama sehemu ya mkakati wake wa kuimarisha maendeleo ya rasilimali watu nchini kote.

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango (wapili kulia), akimkabidhi Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay (wapili kushoto), Tuzo ya Mwajiri Bora 2022 baada ya NMB kuibuka mshindi wa jumla katika hafla ya utoaji tuzo hizo zinazoratibwa na Asasi cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako na kulia ni mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa ATE, Jayne Nyimbo.

“Tunasikia furaha kuibuka mshidi wa jumla leo. Lengo letu ni kuendelea kuinua kiwango na kubaki kuwa mwajiri bora zaidi nchini Tanzania. Baada ya kupata heshima hii, tunashukuru kusherehekea tuzo hizi za thamani kabisa kwetu na tuzo hizi zisingepatikana bila kazi kubwa ya viongozi wetu katika kuongoza maono na juhudi kubwa za wafanyakazi katika Benki yetu katika maeneo yao ya kazi,” Akonaay alisema.

“Tuzo hizi ni kielelezo cha matokeo ya uwekezaji ambao benki  inafanya kwa watu wake. Tuzo hii inathibitisha uwepo wa ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi na inathibitisha zaidi ari ya kujituma kwa wafanyakazi inayotokana na ushirikishwaji katika maamuzi” aliongeza.

Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako alisema Serikali imedhamiria kuboresha maslahi ya watumishi wa sekta binafsi baada ya kupitisha kima cha chini cha mishahara kwa watumishi wa sekta binafsi ambacho kitaanza kutumika rasmi Januari 1, 2023.

“Kima cha chini cha mshahara kwa sekta kibinafsi kimeshapitishwa na kitaanza kutumika Januari 1, 2023. Tumeshirikisha sekta binafsi ipasavyo na ni imani yangu kuwa waajiri wote wa sekta binafsi watazingatia ipasavyo,” alisema.

Mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo hizo alikuwa, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango ambaye aliwataka waajiri kuzingatia sheria za kazi za nchi na kuongeza kuwa ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi juu ya unyanyasaji kutoka kwa waajiri.

“Ofisi yangu imepokea malalamiko kadhaa kutoka kwa wafanyakazi. Nachukua nafasi hii kuwakumbusha waajiri kufanya kazi kwa mujibu wa sheria za kazi za Tanzania. Haki ikicheleweshwa ni kunyimwa haki,” alisisitiza.

Dk Mpango wakati wa hafla hiyo alizitaka kampuni za kimataifa mbalimbali zinazofanya kazi nchini kuzingatia kanuni za sharia za kazi nchi kwa kutoa kipaumbele kwa Watanzania wakati wa mchakato wa ajira na kuongeza kuwa wafanyakazi wa kigeni wanapaswa kuajiriwa haswa ambapo ujuzi haupatikani kwa urahisi nchini.

1 Comment

  • Vigezo ni nini?
    Tuache tabia ya kusifiana wakati hatuna maendeleo ya kutajirisha wananchi na thamani ya shilingi yetu.
    Mbona nchi zilizoendelea hazina tuzo hizi?
    Weka hisa za benki DSE wazawa wanunue.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Habari Mchanganyiko

Makonda autaka mgodi kubadilisha maisha ya wana-Geita

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametoa wito kwa...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Je, miji ya Uingereza inafilisika?

Spread the loveMNAMO 1890, mwandishi mmoja wa habari Mmarekani aitwaye Julian Ralph...

error: Content is protected !!