Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TARURA yazitaka Serikali za Mitaa kutenga bajeti ya barabara
Habari Mchanganyiko

TARURA yazitaka Serikali za Mitaa kutenga bajeti ya barabara

Spread the love

MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seif ameziomba Mamlaka za Serikali za Mitaa mkoani Tabora  kuendelea kutoa ushirikiano  hasa  wakati wa kuandaa bajeti ili kuhakikisha barabara zenye changamoto ambazo ni muhimu zinapewa kipaumbele kwa kutengewa fedha ili zifanyiwe matengenezo na kupunguza adha kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Seif ametoa kauli hiyo jana tarehe 2 Disemba, 2022 alipotembelea barabara ya Mpandamlowoka-Mwaharaja na Kazaroho-Mpandamlowoka zenye urefu wa Km 90.

Baranara hizo zilizopo wilayani Kaliua zipo  katika hatua za matengenezo na zitengenezwa kwa kuzingatia ubora ili kuhakikisha wananchi wanafikia huduma za kijamii.

Mtendaji huyo ametembelea barabara  hizo zilizopo wilayani Kaliua mkoani Taborw ikiwa zimepita siku chache baada ya Waziri wa Nchi-OR TAMISEMI, Angellah Kairuki alipomuagiza afike eneo hilo ili kukagua na kutafuta namna ya kutatua changamoto za barabara hizo.

“Nimefika eneo hili ili kujionea namna hali ilivyo ili kuchukua hatua za haraka na za muda mrefu kwa ajili ya kutatua changamoto ya usafiri kwa wakazi wa maeneo haya ili waweze kufikia huduma za kijamii na kuendelea na shughuli zao za kichumi.

“Nimekuta mkandarasi anaendelea na kazi lakini analegalega, hivyo nimetoa maagizo kwa Meneja wa TARURA Wilaya amsimamie mkandarasi kwa karibu ili  barabara ziweze kupitika kabla ya mwezi Desemba kuisha ”, alisema Mhandisi Seff.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Paul Chacha amemshukuru Mtendaji Mkuu wa TARURA kufika eneo hilo na kuona hali halisi na kueleza umuhimu wa barabara hizo kwa kuwa zinaunganisha barabara kuu ya kwenda Kahama ambayo inawasaidia wananchi kusafirisha mazao yao hasa mpunga na pia barabara zote mbili zinapita maeneo ya mbuga.

Aidha,  wananchi wa Kaliua wameushukuru uongozi wa TARURA kwa kutembelea eneo hilo na kuleta suluhisho la adha kubwa walizokuwa wanazipata.

“Tunaishukuru Serikali kwa kutuona wananchi wa maeneo haya, kwa kweli adha tunazopata ni kubwa sana kwenye usafiri wananchi tunalazimika kutumia gharama kubwa ya usafiri ambapo nauli kwa sasa ni shilingi elfu 35 hadi shilingi elfu 40, sasa tunafurahi serikali imetuona na tunaomba ituboreshee barabara hizi”, alisema Philbert Agostino mkazi wa Kaliua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yapata tuzo ya mwezeshaji bora wa mikopo serikali Afrika

Spread the loveBenki ya NBC imepata tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Pamoja...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!