Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wananchi Musoma Vijiji waanza kupata maji waliyosubiri toka 2013
Habari Mchanganyiko

Wananchi Musoma Vijiji waanza kupata maji waliyosubiri toka 2013

Spread the love

 

WANANCHI wa vijiji vya Chitare na Makojo vilivyoko katika Jimbo la Musoma Vijijini wameanza kupata huduma ya maji safi na salama, baada ya mradi wa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria, kuanza kukamilika tangu ulipoanza kujengwa 2013. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tarime … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 2 Desemba 2022 na Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo.

“Vijiji vya Chitare na Makojo vya Kata ya Makojo, vimesubiri maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria tokea Mwaka 2013. Mradi huu ulioanzwa kutekelezwa na Halmashauri yetu (Musoma DC) tokea Mwaka wa Fedha 2013/2014, sasa unarudiwa na unakamilishwa kwa ubora mzuri na RUWASA,” imesema taarifa hiyo na kuongeza:

“RUWASA inaendelea kujenga miundombinu yenye ubora na sasa wanakijiji wa Chitare, wameanza kupata maji safi na salama ya bomba.Kwa muda mfupi ujao wanakijiji wa Makojo nao watapata maji ya bomba hilo. Tumeomba bomba hilo lijengwe hadi Kijiji cha Chimati ambacho nacho kiko ndani ya Kata ya Makojo. Serikali imepokea ombi letu na kukubali kulitekeleza.”

Wanakijiji wa vijiji hivyo wameishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kufanikisha utekelezaji wa mradi huo, wakisema imeondoa changamoto ya maji iliyokuwa inawakabili kwa muda mrefu, ambapo walikuwa wanafuata maji ziwani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari Mchanganyiko

Prof. Mbarawa aanika mafanikio ya TMA

Spread the loveSHUGHULI za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), zimeimarika...

error: Content is protected !!