Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Tazama hapa matokeo ya Darasa la Saba 2022
ElimuTangulizi

Tazama hapa matokeo ya Darasa la Saba 2022

Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Athumani Salumu
Spread the love

 

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) leo Alhamisi limetangaza matokeo ya darasa la saba ambapo jumla ya watahiniwa 1,730,402 kati ya watahiniwa 1,348,073 wenye matokeo ambao ni sawa na asilimia 79.62 wamefaulu ambako wamepata madaraja A, B, C. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Athumani Salumu amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 558,825 sawa na asilimia 78.91 ya wasichana wenye matokeo na wavulana ni 514,577 sawa na asilimia 80.41 ya wavulana wenye matokeo.

Akitangaza matoke ohayo jijini Dar es Salaam, Salumu amesema; “Ikilinganishwa na mwaka 2021, kitakwimu kuna punguo la ufaulu kwa asilimia 2.35 japokuwa idadi ya watahiniwa waliofaulu imeongezeka kwa 165,600 sawa na asilimia 18.24 ikilinganishwa na mwaka 2021,” NECTA.

Aidha, NECTA imefuta matokeo yote ya watahiniwa 2,194 sawa na asilimia 0.16 ya watahiniwa milioni 1.35 waliofanya mitihani, ambao wamebainika kufanya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!