Thursday , 2 February 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Darasa la saba 2022 wafeli kiingereza
Elimu

Darasa la saba 2022 wafeli kiingereza

Wanafunzi wa darasa la saba wakifanya mtihani
Spread the love

 

MATOKEO ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) 2022 yanaonesha kuwa ufaulu wa watahiniwa katika masomo yote uko juu ya wastani isipokuwa kwa somo la Kiingereza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa tathmini ya awali ya matokeo hayo yaliyotangazwa leo tarehe 1 Disemba, 2022 na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), kwa upande wa somo la hilo la Kiingereza jumla ya watahiniwa 59,990 (4.45%) wamepata Daraja la A.

Watahiniwa 56,569 (4.20%) wamepata Daraja la B, watahiniwa 279,580 (20.74%) wamepata Daraja la C, watahiniwa 912,708 (67.71%) wamepata Daraja la D wakati waliopata Daraja la E ni 39,086 sawa na asilimia 2.90.

Aidha, takwimu za somo la Hisabati zinaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 43,362 (3.22%) wamepata Daraja la A, watahiniwa 133,288 (9.89%) wamepata Daraja la B, watahiniwa 541,623 (40.18%) wamepata Daraja la C, watahiniwa 613,442 (45.51%) wamepata Daraja la D na waliopata Daraja la E ni 16,267 sawa na asilimia 1.21.

Somo la Sayansi na Teknolojia jumla ya watahiniwa 67,071 (4.98%) wamepata Daraja la A, watahiniwa 287,690 (21.34%) wamepata Daraja la B, watahiniwa 610,839 (45.31%) wamepata Daraja la C, watahiniwa 360,031 (26.71%) wamepata Daraja la D na waliopata Daraja la E ni 22,362 sawa na asilimia 1.66.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuMakala & Uchambuzi

Waraka maalumu kwa NECTA, “hawapaswi kuungwa mkono”

Spread the loveHATUA iliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), ya...

Elimu

NACTVET yafungua dirisha la udahili

Spread the love  BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo...

Elimu

Prof. Mwakalila awafunda wanafunzi Chuo Mwalimu Nyerere, “ulipaji ada ni muhimu”

Spread the love  MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere (MNMA),...

ElimuMakala & UchambuziTangulizi

Shule ya msingi yajengwa miaka 25 bila kukamilika, wanakijiji wachoka kuchangia

Spread the love  Wakazi wa Kijiji cha Makomba kilichopo kata ya Makazi...

error: Content is protected !!