Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Bashe asema Tanzania haina njaa, akiri bei juu ya mazao
Tangulizi

Bashe asema Tanzania haina njaa, akiri bei juu ya mazao

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe
Spread the love

 

WAZIRI wa Kilimo nchini Tanzania, Hussein Bashe, amekanusha uwepo wa baa la njaa nchini humo lakini amekiri kupanda kwa bei za mazao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara … (endelea).

Bashe amesema bei ya mazao imepanda kwasababu ya maamuzi ya Rais wa nchi hiyo kuifanya sekta ya kilimo kuwa sekta ya kibiashara.

Waziri huo ametoa kauli hiyo leo Jumatano tarehe 23 Novemba, 2022, katika ziara ya Rais Samia Suluhu mkoani Manyara.

Hata hivyo amesisitiza umuhimu wa kujiwekea akiba ya chakula ambapo amesema Serikali imeendelea na jitihada za kuonbgeza uwezo wa kuhifadhi chakula kutoka tani 200,000 kufika tani laki 500,000.

Jana Rais Samia alishuhudiwa akizindua vihenge vikubwa vya kuhifadhia nafaka ambavyo vitasaidia kuongeza uwezo wa hifadhi ya Taifa ya chakula.

Bashe amesema pale bei ya chakula inapopanda Serikali hutumia hifadhi iliyopo kuongeza upatikanaji ili kupunguza ushindani kwenye soko na hivyo bei kupungua.

“Leo nimezunguka hapa babati b=debe la mahindi limefika Sh 20,000, Serikali inachofanya ni kuchukua mazao na kupeleka sokoni na kuuza kwa bei ya chini. Tutafanya hivyo, tutakifungulia,” amesema.

Amefafanua kuwa wataalamu wa kilimo wanafanya tathimini na kwamba watauza mahindi katika maeneo maalumu kwa bei ya rejareja na si kwa wafanyabiashara wakubwa.

Amesema mahindi hayo yatauzwa kwa bei ya Sh 700-800 kwa kilo sawa na Sh 14,000-15000 kwa debe moja la mahindi.

“Serikali kazi yake sio kuua soko bali kufanya hatua ambazo zitafanya wananchi wapate unafuu bila kumtia umasikini mkulima,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!