Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa TLP yampata anayekaimu nafasi ya Mrema
Habari za Siasa

TLP yampata anayekaimu nafasi ya Mrema

Hamadi Mkadamu (kushoto)
Spread the love

 

SEKRETARIETI ya chama cha TLP imemchagua aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Hamadi Mkadamu kuwa kaimu mwenyekiti taifa wa chama hicho kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti Agustino Mrema. Anaripoti Juliana Assenga, UDSM … (endelea).

Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo uliofanyika leo tarehe 9 Septemba, 2022, makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TLP, Richard Lyimo, Sekretarieti ya chama imewashindanisha Mkadamu na Makamu Mwenyekiti Taifa Bara, Dominata Rwechungura.

Katibu Mkuu amesema Sekretarieti ya chama ina jumla ya wajumbe kumi na waliohudhuria kikao hicho ni Makamu Mwenyekiti(zanzibar) Hamadi Mkadamu, Makamu Mwenyekiti(Rechengura,Naibu katibu Mkuu(zanzibar) Hussain Juma, Naibu katibu Mkuu Michael mrema, Naibu katibu Mkuu utawala Rwamugira.

Katibu Mkuu huyo amesema chama wamekutana na kuwapigia kura makamu wawili Dominata Rwechungnura(Bara) na Alhaji Hamadi Mkadamu(visiwani).

Amesema matokeo ya uchaguzi wa kati ya makamu hao wawili Hamad Mkadamu ndiye aliyeweza kuchaguliwa kushikilia nafasi hiyo ya uenyekiti taifa.

Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema akifungua mkutano mkuu.

Richard pia amesema kwa kurejelea katiba ya TLP inayo mikutano mikuu miwili ambayo ni mkutano wa dharura na mkutano wa kikatiba.

Lyimo amesema kutokana na kutokuwepo kwa mwenyeketi chama kilishindwa kuitisha mikutano yake lakini mara baada ya kuwa amekwisha patikana Mwenyekiti wa muda watapanga ni lini kuita mkutano mkuu kwa ajili ya kumchagua rasmi mwenyekiti wa chama hicho.

Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa Hamad amewashukuru wajumbe kwa kumchagua kukaimu nafasi hiyo mpaka pale atakapochaguliwa Mwenyekiti mwingine.

Hamad amesema kuwa atakuwa tayari kushirikiana na wajumbe wengine katika kuendeleza nyayo zake aliyekuwa mwenyekiti Agustino Mrema bila ya kwenda kinyume.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!