Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rahabu Jackson ashinda nyumba ya milioni 200
Habari Mchanganyiko

Rahabu Jackson ashinda nyumba ya milioni 200

Spread the love

KAMPUNI ya simu ya kiganjani – Vodacom imetoa  zawadi ya nyumba yenye thamani ya Sh.milioni 200 na samani za ndani zenye thamani ya Sh. milioni 60 kwa Rahabu Jackson – mshindi aliyeshinda kampeni ya ‘M-pesa Imeitika’. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma… (endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 9 Septemba mwaka huu na Mkurugenzi wa Vodacom na M-Pesa Tanzania, Epimack Mbetini alipokuwa akizungumzia na wananchi wa Dodoma waliopo katika nyumba za mradi wa shirika la nyumba Tanzania NHC Iyumbu.

Mbetini ameeleza kuwa kampuni huyo ambayo inalenga kuboresha maisha ya watu imekuwa ikitoa zawadi mbalimbali kwa watumiaji wa mtandao huo bila kujali jinsia, dini, kabila wala hali ya mtu ilimradi mteja anatumia mtandao huo kwa kufanya malipo mbalimbali ya kiserikali pamoja na manunuzi ya kawaida.

Amesema katika kaulimbiu ya M-imeitika kampuni imeutoa zawadi kwa vijana kwa kuwapatia bajaji, bodaboda pamoja na zawadi kubwa ambayo ni nyumba huku akieleza kuwa zaidi ya asilimia 99.9 ya washindi ni akina mama.

“Kampuni ya Vodacom Tanzania imekuwa ikifanya mashindano kwa watumiaji bora kwa huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo

“Kampuni yetu imefanya ubunifu wa kuanzisha mashindano ya ‘M-Pesa imeitika’ kwa lengo la kutoa zawadi mbalimbali kwa kuinua uchumi wa wateja wetu sambamba na kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupunguza tozo mbalimbali ambazo zilikuwa zikionekana kuwafanya wateja kukwepa matumizi ya miamala.

“Kutokana hali hiyo wananchi kwa sasa wameanza kufurahia utumiaji wa mtandao kwa kufanya malipo mbalimbali ambapo kwa sasa wateja wanaanza kurejea.

“Sambamba na hilo Vodacom kwa sasa inatoa Sh. Bilioni 100 kila mwezi kwa ajili ya kuwaongezea mitaji mawakala jambo ambalo linaendelea kuwafanya vijana kujikwamua” ameeleza Epimack.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri amesema mitandao ya kijamii imesaidia kuongeza pato la Taifa pamoja na kufanya maendeleo kwa vijana pamoja na kuimarisha uchumi wa watanzania hususani vijana.

“Pamoja na kutoa zawadi mbalimbali lakini huduma ambazo zinatolewa na kampuni ya Vodacom Tanzania zimekuwa zikisaidia upatikanaji wa huduma kwa rahisi na kuepukana na matumizi ya kutembea na pesa mkonono” ameeleza Shekimweli.

Muda mfupi kabla ya kukabidhi nyumba kwa mshindi Katibu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Alan Kijazi amesema kampuni hiyo imekuwa ikijitahidi kwenda kwa kasi pamoja na kuwa wabunifu na ndiyo maana imekuwa ya kwanza kuingiza mfumo wa 5G hapa ncjini.

Hata hivyo, amewataka kuendelea kuwa wabunifu kwa mambo mbalimbali kwasababu hivi sasa ulimwengu unabadilika na mambo yanaenda kwa kasi.

Naye mshindi wa nyumba hiyo Rahabu Jackson mkazi wa Manyoni mkoani Singida ameeleza furaha yake huku akisema alikuwa akitumia miamala kwa kutuma pesa kununua umeme na huduma nyingine mbalimbali.

“Kwakweli ninayo furaha ya kutosha sijawahi kutegemea kama nitashinda kwa zawadi kubwa kama hii, nilikuwa nikifanya kama mchezo na sijawahi kutumia pesa nyingi bali nilikuwa nikituma pesa kidogo kwa ndugu, kufanya malipo mbalimbali pamoja na kununua bando.

“Nilipigiwa simu na sikuwa mwepesi kuisikiliza kwani nilidhani ni matangazo ya Vodacom lakini niliamua kuweka sauti ya nje na kusikiliza na ndipo nilipobaini kuwa ni sauti halisi ya watu na siyo ile ya kurekodiwa.

“Nilipoambiwa kuwa nimeshinda nyumba kwakweli sikuamini lakini sasa ikawa kweli na sasa nimekabidhiwa hivyo nawashauri watanzania washiriki mashindano hayo yatakayoendelea kwani ukweli mwenye bahati atafanikisha” ameeleza Jakson.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!