Saturday , 4 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT Wazalendo kumjadili mgombea EALA, uchaguzi mkuu
Habari za Siasa

ACT Wazalendo kumjadili mgombea EALA, uchaguzi mkuu

Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu
Spread the love

 

CHAMA cha ACT-Wazalendo kinatarajia kufanya kikao cha Halmashauri Kuu tarehe 4 Septemba mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine kitaidhinisha jina la Mgombea wa Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA). Anaripoti Felister Mwaipeta, TUDARCo … (endelea).

Pia kikao hicho kitakachohudhuriwa na viongozi mbalimbali, kitajadili mkakati wa chama hicho kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka 2024 pamoja na uchaguzi mkuu mwaka 2025.

Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa leo tarehe 30 Agosti, 2022 na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma ya chama hicho, Janeth Rithe.

Rithe alisema kikao hicho kikitanguliwa na vikao vya siku mbili vya Kamati kuu utakaofanyika tarehe mbili na tatu Septemba jijini Dar es Salaam.

“Kikao cha Halmashauri Kuu kitajadili ujenzi wa chama kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 na Uchaguzi mkuu wa 2025 hasa ikizingatiwa tumejipanga kikimilifu kuelekea uchaguzi huo,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!