Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Michezo Samia awapongeza Simba Queen kutwaa CECAFA
Michezo

Samia awapongeza Simba Queen kutwaa CECAFA

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan ameipongeza Klabu ya Soka ya Simba Qeens SC kwa kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki wa CECAFA 2022 kwa Wanawake (SAMIA CUP). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Mmejenga heshima kwa soka la Tanzania na nchi kwa ujumla. Nawatakia kheri katika Ligi ya Mabingwa Afrika (2022 CAF Women’s Champions League ) itakayofanyika nchini Morocco.

Rais Samia ametoa pongezi hizo leo tarehe 28 Agosti, 2022 baada ya timu hiyo ya Simba Queens kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya She Corporates ya Uganda usiku wa jana katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la dar es Salaam.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Rais Samia ameandika, “Nawapongeza wanangu Simba Qeens SC kwa ubingwa wa Afrika Mashariki wa CECAFA 2022 kwa Wanawake (SAMIA CUP). Mmejenga heshima kwa soka la Tanzania na nchi kwa ujumla. Nawatakia kheri katika Ligi ya Mabingwa Afrika (2022 CAF Women’s Champions League) itakayofanyika nchini Morocco”.

Bao pekee la Simba lilitiwa kimyani na kiungo wa kimataifa wa Kenya, Vivian Corazone Aquino Odhiambo dakika ya 49 kwa penalti baada ya Asha Djafar kuangushwa kwenye boksi.

Timu hiyo ya Simba Queen itauwakilisha ukanda wa CECAFA kwenye Ligi ya mabingwa ya wanawake Oktoba mwaka huu nchini Morocco.

Pamoja na ushindi huo, Simba Queens pia wametoa kipa Bora wa mashindano, mzawa Gelwa Yona na Mchezaji Bora wa Mashindano, ambaye ni Vivian Corazone Aquino Odhiambo, huku Abela Roza wa Commercial Bank ya Ethiopia akiwa Mfungaji Bora.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Uingereza, Hispania, Italia na Ufaransa kinawaka leo

Spread the loveLIGI mbalimbali barani ulaya kuendelea leo na michezokadhaa mikali itakwenda...

Michezo

Leo mkwanja upo Meridianbet, usipishane nao

Spread the love  Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Michezo

Anza wikendi yako na Meridianbet, upige mkwanja wa maana

Spread the love Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Habari MchanganyikoMichezo

Arafat atoka bima na kurejea kwenye benki

Spread the loveRais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amemteua Arafat Ally Haji kuwa...

error: Content is protected !!