Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Michezo KMC yatua Arusha kibabe
Michezo

KMC yatua Arusha kibabe

KMC
Spread the love

 

KIKOSI cha KMC imetua jijini Arusha kwa maandaizi ya michezo yake miwili ya Ligi Kuu ya NBC, msimu wa 2022/23 itakayopigwa tarehe 17 na 21 Agosti, mwaka huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini humo. Anaripoti Damas Ndelema, TUDARCo … (endelea).

Timu hiyo ilioyo chini ya kocha, Thiery Hitmana imeondoka jana ikiwa na jumla ya wachezaji 24 huku nyota wake watatu wapya wakisalia jijini Dar es Salaam na wataukosa mchezo huo baada ya kupata majeraha wakati wakiwa mazoezini na wachezaji hao ni Blaise Bigrimana, Waziri Junior, na Eric Manyama

Kupitia taarifa iliyotolewa na Afisa habari na Mawasiliano wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wamejiandaa vya kutosha na wamekuja Arusha kwa ajili ya kuchukua alama sita katika michezo yote miwili aidha pia wanafahamu kuwa ushindani ni mkubwa kutokana na kila timu imejiandaa vya kutosha.

“Tumekuja kupata alama sita kwenye michezo hii miwili tunajua ushindani ni mkubwa kutokana na jinsi timu zilivyo jiandaa pia tunahitaji ushindi kwa ni jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wetu,” alisema Afisa huyo.

Aidha hapo awali kwa mujibu wa ratiba KMC ilitakiwa kuanzia ugenini katika uwanja wa mkwakwani dhidi ya Coastal Union kisha kusafiri mpaka Moshi kucheza na Polisi Tanzania katika uwanja wa Ushirika lakini kutokana na taarifa ya kufungiwa kwa viwanja hivyo ikapelekea kupangwa katika uwanja huo wa Sheikh Amri Abed uliopo jijini Arusha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa tu kutoka Meridianbet

Spread the love  IKIWA leo hii ni Jumamosi nyingine na tulivu kabisa,...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

error: Content is protected !!