Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Michezo Ngao ya Jamii kuchezwa kwa mtoano
Michezo

Ngao ya Jamii kuchezwa kwa mtoano

Spread the love

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza mabadiliko ya kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara zitakazotumika katika msimu ujao wa 2022/23 ambapo kuanzia msimu ujao michuano ya Ngao ya Jamii huwa maalum kwa ajli ya ufunguzi wa msimu mpya wa itachezwa kwa njia ya mtoano na ndipo bingwa anapatikana. Anaripoti Damas Ndelema, TUDARCo … (endelea).

Mashindano hayo yaliyokuwa yakichezwa kwa mfumo wa mechi moja ambapo bingwa wa Ligi Kuu atacheza na bingwa wa Kombe la Shirikisho na endapo bingwa wa Ligi Kuu atakuwa ndiyo bingwa wa Shirikisho basi mshindi wa pili katika ligi atapata nafasi ya kushiriki michuano hiyo na itachezeka mechi moja kisha bigwa kupatikana.

Kupitia taarifa hiyo iliyotolewa na Bodi ya Ligi inaeleza kuwa mashindano hayo yataanza kufanyika kwa timu tatu zinazoshika nafasi tatu za juu katika msimu wa ligi kuu na bingwa wa Kombe la Shirikisho endapo bingwa wa shirikisho atakuwa mmoja wa timu tatu za juu basi nafasi itajazwa na timu iliyoshika nafasi ya nne kwenye msimamo na kisha mashindano kufanyika kwa njia ya mtoano na bingwa kupatikana.

Aidha kanuni hii itaanza kutumika kuanzia ufunguzi wa Ligi ya msimu ujao ambapo katika ufunguzi wa msimu huu tayari ushafanyika na klabu ya soka ya Yanga kufanikiwa kuibuka bingwa baada ya kuifunga klabu ya Simba kwa mabao mawili kwa moja na kutwaa ubingwa huo mara ya pili mfululizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!