Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Samia: Vijana njooni kwenye kilimo
Habari MchanganyikoTangulizi

Samia: Vijana njooni kwenye kilimo

Spread the love

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ametoa wito kwa vijana kuwekeza kwenye sekta ya kilimo kutoka na fursa nyingi zilizopo na uboreshwaji wa mazingira ya kilimo unaondelea kufanywa na Serikali. Anaripoti Jonas Mushi Dar es Salaam…(endelea).

Mkuu huyo wa nchi ametoa wito huo leo tarehe 8 Agosti 2022 katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima maarufu Nane Nane yaliyofanyika Kitaifa mkoani Mbeya.

“Katika kuongeza ajira kwa vijana tarehe 3 Agosti Waziri Mkuu alizindua mradi wa kuwezesha vijana katika kilimo vijana njooni kwenye sekta ya kilimo, tumejipanga kuwapatia mashamba na mashamba hayo yatakuwa na hati zitakazotoka kwa majina ya vijana watakaokuja iwe makundi au mmoja mmoja,” amesema Samia.

Amesema Serikali imejipanga kuwaunga na mabenki ili kupata mikopo nafuu, “mabenki yapo tayari kuna fedha ambazo wameziweka kwaajili hiyo.”

Pia amesema Serikali imejipanga vizuri kutafuta masoko “kila tutakachokizalisha tayari kina soko, ziara ninazozifanya nje ya nchi nikwenda kutafuta masoko ya bidhaa tunazozalisha na tayari masoko yapo tunasubiriwa sisi uzalishaji ili tuweze kupeleka.”

Amesema amefurahishwa sana wakati na vijana ambao tayari wamejiweka kwenye kilimo katika sekta tofauti ambao amewaona katika maonesho hayo “na wana ari kubwa ya kufanya kazi hiyo.”

Amesema takwimu kutoka benki ya Dunia na Shirika la Chakula Duniani FAO zinaonesha kufikia mwaka 2050 idadi ya watu duniani itafikia bilioni 9, Afrika ikiwa na watu karibu bilioni 2 na Tanzania kufikia watu milioni 100.

Amesema kutokana na hali hiyo mahitaji ya chakula duniani yataongezeka ikiwemo mahitaji ya Tanzania yenyewe.

“Kuongezeka huko kwa idadi ya watu na mahitaji ya chakula ni fursa ya mazao ya chakula ambayo kama nchi tunapaswa kujiandaa kwa mazingira hayo yanayokuja,” amesema.

Amesema kutokana na sekta za kilimo, mifugo na uvuvi kuendelea kuwa muhimili muhimu wa kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi serikali imeongeza bajeti kutoka Sh294 bilioni mwaka 2021/22 hadi Sh 954 bilioni mwaka 2022/23.

“Ongezeko hilo linalenga kutatua changamoto katika maeneo ya utafiti na  uzalishaji wa mbegu bora, umwagiliaji, huduma za ugani na ujenzi wa maghala vijijini ili kufikia lengo la ukuaji wa sekta ya kilimo kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza namna Nathwani alivyomjeruhi jirani yake

Spread the loveMSIMAMIZI wa Msikiti wa Wahindi Lohana aitwae, Ankit Dawda (32)...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!