Monday , 13 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bilioni 14/-kujenga maktaba ya kisasa MNMA
Habari Mchanganyiko

Bilioni 14/-kujenga maktaba ya kisasa MNMA

Spread the love

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amezindua na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Maktaba la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) Kivukoni Jijini Dar es Salaam, mradi ambao utagharimu zaidi ya Shilingi bilioni 14 ili kuboresha mazingira ya Kufundishia na kujifunzia. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo jana tarehe 12 Julai, 2022, Profesa Mkenda alisema mpango wa sasa wa Serikali katika Sekta ya Elimu ni kuzalisha wasomi watakaokuwa na Elimu ya Kujitegemea kwa kuboresha mitaala ambayo mpaka sasa zaidi ya wadau laki moja wamekwisha toa maoni yao.

Prof. Mkenda amesema ubora wa Elimu ni ajenda ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambayo inahitaji mageuzi ili kuongeza ubora na iakisi mahitaji ya nchi, utandawazi kwa lengo la kuongeza uwekezaji.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Francis Maiko amekipongeza Chuo hicho kwa kutenga bajeti kiasi cha asilimia arobaini ambazo ni  fedha za ndani kwa ajili ya miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Hiki kilichofanywa na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kinatakiwa kiwe mfano wa kuigwa na Taasisi nyingine ili kuwezesha Serikali kuendelea kutumia bajeti zinazotengwa kwa lengo la kuboresha zaidi Miundombinu ya Kufundishia na kujifunzia,alisisitiza Prof Mkenda.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila amesema ujenzi wa jengo hilo utakuwa na Maktaba, Ukumbi wa Mihadhara pamoja na ofisi za wafanyakazi.

Tumekusanyika leo hapa kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo la Maktaba lenye uwezo kuchukua wanafunzi 2500, Ukumbi wa Mihadhara wa kutosha Wanafunzi 1000 pamoja na ofisi za Wafanyakazi,alisema Prof. Mwakalila.

Aidha Mchakato wa Mradi huo waa Maendeleo ulianza katika bajeti yam waka 2018/2019, hata hivyo pamoja na kutengewa bajeti ya Maendeleo lakini fedha za miradi ya Maendeleo hazikutolewa hivyo katika bajeti yam waka 2021 Chuo kiliamua kutenga bajeti ya asilimia 40 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Prof. Mwakalila aliitaja miradi mimngine inayosimamiwa na Chuo hicho kuwa ni mradi wa ujenzi wa jengo la hosteli ya Wanafunzi katika Kampasi ya Karume Zanzibar lenye uwezo wa kulaza Wanafunzi 1536 ulioanza Julai 18, 2021 na utagharimu zaidi ya bilioni 15.

Msimamizi wa mradi huo kutoka Wizara ya Ujenzi  Mhandisi Mwesigwa Ichwekeleza alisema mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 5 na utakuwa ni wa ghorofa 3 ambao utakamilika ndani muda wa miezi 30 kama ilivyopangwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Moduli ya kuwasilisha rufaa za zabuni kieletroniki kuanza Julai

Spread the loveMamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imesema moduli...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Mshindi ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ akabidhiwa trekta

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imehitimisha msimu wa tatu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hati Fungani ya NMB Jamii yaanza kuuzwa Soko la Hisa London

Spread the loveBenki ya NMB imetanua wigo wa kushiriki katika masoko ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Vituo 13 vyasitishiwa mkataba madai kutaka kupiga bilioni 4 za NHIF

Spread the loveVITUO vya kutoa huduma za afya 13, vimesitishiwa mikataba ya...

error: Content is protected !!