Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Gesi asilia kuchochea ukuaji wa uchumi mikoa ya kusini
Habari Mchanganyiko

Gesi asilia kuchochea ukuaji wa uchumi mikoa ya kusini

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Uchimbaji Gesi na Mafuta (OGAWOGA), Frank Mwankefu akizungumza na waandishi wa habari
Spread the love

IMEELEZWA kuwa utekelezaji wa Mradi wa Kuchakata Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG), katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania utachochea ukuaji wa uchumi, maendeleo na huduma za kijamii kwa wananchi na mikoa hiyo.

Mradi huo ambao  uwekezaji wake unatarajiwa kuanza mwaka 2025 mkoani Lindi na kukamilika 2030 unagharimu Sh.trilioni 70. Anaripoti Suleiman Msuya… (endelea)

Akizungumza na waandishi wa habari jana tarehe 12 Julai, 2022 katika Banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), lililopo Viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba Temeke jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya PURA Halfani Halfani alisema mradi wa LNG unaenda kufanya mapinduzi kwa wananchi mikoa ya Kusini ambayo ni Lindi, Mtwara na Pwani.

Mhandisi wa Petroli Alexander Gosbert akitoa elimu kwa watawa wa Kituo cha Wadada Wadogo kwenye banda la PURA katika walipotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Viwanja vya Sabasaba wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam.

Halfani alisema mradi wa LNG ukitekelezwa kwa kiwango ambacho kinarajiwa gesi nyingi itazalishwa na kutumika nchini na nyingine kuuzwa nje hivyo kuongeza ajira.

“Katika utelelezaji wa mradi huu ajira zisizo za kudumu zaidi ya 10,000 zitapatikana.Mfano wauza nondo, saruji, kokoto, vyakula na vingine, hivyo mzunguko wa fedha utakuwa mkubwa na mapinduzi ya kiuchumi na jamii yataonekana,”alisema.

Halfani alisema PURA itaendelea kutafuta wawekezaji ambao watawekeza katika eneo la mafuta na gesi ambalo limeonesha mafanikio makubwa katika kuinua uchumi wa nchi nyingi.

Alisema pia PURA inaendelea kuunganisha  kampuni za  Kitanzania ambazo zinazotaka kushiriki utafutaji na uchimbaji gesi na mafuta kupata nafasi.

Mwenyekiti alisema uamuazi wa Serikali kuruhusu uchimbaji wa gesi asilia umewezesha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuwa na uhakika wa nishati ya umeme na ambao unatumiwa na wananchi wengi mjini na vijijini.

Mhandisi wa Petroli Robinnancy Mtitu akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Halfani Halfani alipotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Viwanja vya Sabasaba wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam.

Alisema pia wanahamasisha wananchi kutumia gesi asilia majumbani kwa kuwa ni salama kwa wananchi.

“Mimi nasisitiza majadiliano yaendelee kuwa mazuri, ili lengo la Serikali kuzalisha gesi asilia ya LNG yafanikiwe kama yalivyopangwa,” alisema.

Aidha alisema PURA imekuwa ikishawishi Watanzania kushiriki kwenye miradi mbalimbali ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi ambao mwitikio umeanza kuonekana.

Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni wa Kampuni ya Solution Tag Consultant Limited, Tumain Abdallah alisema PURA imekuwa kiungo muhimu wa wao kupata kazi kwenye miradi ya uchakataji gesi asilia.

Abdallah alisema kwa muda mrefu kampuni za wazawa zilikuwa haziaminiki ila kupitia PURA wameaminika na kupewa kazi za ushauri wa masuala ya mafuta na gesi.

“PURA imewaaminisha wawekezaji kuwa sisi tunaweza na hatujawaangusha, kwani tunaendelea kutoa huduma za masuala ya gesi na mafuta kwa kiwango kikubwa,”alisema.

Alisema kampuni yao  ina wafanyakazi wazawa tisa ambapo ameshauri vijana Wakitanzania ambao wamesoma mambo ya gesi na mafuta kujitokeza kushiriki.

Naye Mwenyekiti wa Wafanyakazi wa Uchimbaji Gesi na Mafuta (OGAWOGA), Frank Mwankefu alisema ujio wa PURA umeweza kuwafanya watambulike na kupata kazi katika miradi ya Songo Songo na kwingine.

“Hii PURA imetufanyia mambo makubwa sisi wachimbaji wa mafuta na gesi, tunaahidi kutowaangusha,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!