Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Vigogo wa Bandari kortini Dar, yumo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu
Habari MchanganyikoTangulizi

Vigogo wa Bandari kortini Dar, yumo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu

Spread the love

 

VIGOGO wanne wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka matatu, likiwemo la kuisababishia serikali hasara ya dola za Marekani 1.8 milioni (sawa na Sh. 4.2 bilioni). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Waliofikishwa mahakamani kwa makosa hayo, ni Ofisa Rasilimali Watu wa mamlaka hiyo, Peter Gawile (58); Mwenyekiti wa Bodi ya Manunuzi, Casmily Lujegi (65); Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi, Mashaka Kisanta (59) na Kilian Chale (51), ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Mshitakwa mwingine, Madeni Kipande, ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, hakuwepo mahakamani kusomewa mashitaka yake, kutokana na kufanyiwa upasuaji wa mgongo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI).

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali Timotheo Mmari, leo 30 nJuni 2022, imedaiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhan Rugemalira, kuwa kati ya tarehe 1 Oktoba 2014 na 1 Oktoba 2020, jijini Dar es Salaam, washitakiwa walikula njama na kuisababishia hasara TPA.

Aidha, kati ya tarehe 1 Januari 2015 hadi 17 Februari 2015, washitakiwa wakiwa maofisa wa TPA, walitumia madaraka yao vibaya kwa kutangaza zabuni Na. AE/016/2014-15/CTB/G/39 kwa nia ya kujipatia dola za Marekani 1,857,908.04 .

Vilevile, katika kipindi hicho cha 2014 na 2020, wakiwa huko TPA na maeneo mengine jijini Dar es Salaam, washitakiwa kwa makusudi walitangaza zabuni ya Enterprises Planning Resources (ERP), bila kupata kibali cha Bodi ya zabuni ya mamlaka.

Mbali na tuhuma hiyo, wote kwa pamoja, wanadaiwa kushindwa kufuata kanuni za zabuni na hivyo kutoa malipo ya awali ya asilimia 40 bila idhini ya Bodi, jambo lililosababisha TPA hasara hiyo.

Washitakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida kusikilizwa mahakama Kuu ama kupata kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Upande wa mashitaka umeileza Mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo, bado haujakamilika na hivyo kesi imeahirishwa hadi 14 Julai mwaka huu.

Kwa upande mwingine, Hakimu Rugemalira alihoji upande wa mashitaka sababu za kuwaleta washitakiwa mahakamani wakati upelelezi hujakamilika, kwani watuhumiwa wanapaswa kufikishwa mahakamani wakati upelelezi ukiwa umekamilika, ili kuanza kusikiliza shauri husika na haki kutendeka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari Mchanganyiko

Prof. Mbarawa aanika mafanikio ya TMA

Spread the loveSHUGHULI za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), zimeimarika...

error: Content is protected !!