Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Jaji Mkuu awapa angalizo watumishi wanaoihama Mahakama
Habari Mchanganyiko

Jaji Mkuu awapa angalizo watumishi wanaoihama Mahakama

Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma
Spread the love

 

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, amewapa angalizo watumishi wa mahakama wanaohama kwa sababu ya maslahi, akisema siku maslahi ya mahakama yatakapoboreshwa wakitaka kurudi watakumbushwa kwamba walikimbia majukumu yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Prof. Juma ametoa kauli hiyo leo Jumatano, tarehe 29 Juni 2022, akifungua mkutano wa tatu wa Baraza Kuu la Saba la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania, uliofanyika jijini Dodoma.

“Pamoja kwamba ni haki ya mtumishi kuhama taasisi ya umma kwa kufuata utaratibu, bado mimi nashangaa wanaofikiri kuondoka mahakama waende sehemu nyingine yenye maslahi mazuri kwa sababu naamini maslahi yetu yakishakuwa bora watatamani kurudi,” amesema Prof. Juma.

Prof. Juma amesema “tunaboresha, watakaoondoka mkirudi tutawakumbusha kwamba mlitukimbia.”

Mkuu huyo wa Mahakama ya Tanzania, amesema wanaofanya vitendo hivyo siyo watumishi bali ni wafanyakazi na kwamba wanachoangalia ni maslahi yao binafsi.

“Watu kama hao sio watumishi bali ni wafanyakazi na wanachoangalia zaidi maslahi yao binafsi, kwa hiyo tusiwe wafanyakazi tuwe watumishi ambao tunaangalia picha kubwa zaidi ambayo ni ustawi wa haki, utawala bora na sisi tunaamini tuna mchango mkubwa sana katika shughuli zetu za kila siku,”amesema Prof. Juma.

Prof. Juma amewataka watumishi wa mahakama kuwa wavumilivu wakati Serikali ikiboresha maslahi yao.

“Shughuli zetu hazilingani kabisa na malipo tunayopata, ukijilinganisha na wale waliopo sekta binafsi waliosoma kama ninyi wana malipo makubwa zaidi lakini sisi tunajivunia hiyo picha kubwa ya ustawi wa Watanzania wengi kuliko ustawi wa biashara zetu,” amesema Prof. Juma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yapata tuzo ya mwezeshaji bora wa mikopo serikali Afrika

Spread the loveBenki ya NBC imepata tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Pamoja...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!