Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Je, Wamiliki wa kumbi za starehe wanawalenga wanafunzi wa vyuo?
ElimuMakala & Uchambuzi

Je, Wamiliki wa kumbi za starehe wanawalenga wanafunzi wa vyuo?

Spread the love

 

KUNA usemi usemao “usilolijua ni sawa na usiku wa giza”  na  ndivyo wamiliki wa kumbi za starehe maeneo yaliyo karibu na vyuo au sehemu wanazo patikana wanafunzi kwa wingi wameiweka jamii katika kiwi kizito wakishindwa kung’amua fumbo hilo zito. Je, lengo lao ni kupata wateja wengi ambao ni wanafunzi ama wana lengo la kufanya biashara bila kuwalenga wanafunzi? Anaripoti Victoria Mwakisimba, TUDARco … (endelea).

Eneo la Mwenge lipo karibu na vyuo mbalimbali kama vile TUDARCo, Ustawi wa jamii, Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Chuo kikuu cha Ardhi na chuo cha Uhasibu. Wanafunzi kutoka vyuo hivi asilimia kubwa wanaishi karibu na vyuo vyao na maeneo hayo ni Mwenge na Sinza.

Ni ukweli usiopingika kwamba wanafunzi wakiwa mbali na makwao wanakuwa huru sana, hakuna anaye wapangia muda wa kutoka wala kuingia na hapa ndipo linapo ibuka wimbi kubwa la wanafunzi wanaokengeuka na kubadili mwenendo kwa kuanza kuwa walevi na wengine kuanza kwenda kwenye kumbi za starehe”.

Mwandishi amezungumza na mfanyakazi ndani ya “club” moja hapo  Mwenge aliyeomba jina lake lihifadhiwe anasema” ni kweli wateja wengi ni wanafunzi kutoka vyuo vya karibu lakini siku za ijumaa , jumamosi na jumapili wateja wanafunzi huwa wengi zaidi ndani ya club hiyo”

Kwa upande wa wanafunzi mwandishi alipata taarifa pia ya wanafunzi wanaoishi eneo jirani na club hiyo na wakathibitisha wanafunzi wenzao huwa wanaenda hapo kwa wingi sana.

Hatuwezi kuwalaumu wamiliki wa kumbi hizo moja kwa moja lakini uwepo wa kumbi hizo umechochea madhara makubwa kwa wanafunzi, badala ya kuzingatia masomo wametekwa na ujana wa kupenda starehe hali inayo hatarishi maendeleo yao kitaaluma.

Lakini si hivyo tu pia maadili hayapo tena kwa wanafunzi kadiri wanavyozidi kuhudhuria na kutumbukia kwenye anasa ndivyo wanavyozidi kufanya uovu mwingi amabao ni hasara kwao na taifa.

Hali si hali tena wanafunzi wanazidi kuangamia je nini kifanyike sasa ,wanafunzi wapewe elimu zaidi juu ya madhara makubwa wanayopata kupitia anasa hizo? Au kumbi zisijengwe tena karibu na maeneo yao ili wasishawishike kirahisi? Hii ndio sintofahamu iliyopo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miaka 28 watumishi UDSM yaliwa na nzige, madumadu

Spread the loveGEORGE Francis anasikitika; anatembea akiwa na mawazo mengi, hajui la...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nimekumbuka Samia wa miaka 3 iliyopita

Spread the loveWAKATI naandaa makala ya safu hii wiki hii, nimejikuta nakumbuka...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Hakuna fedha za Rais

Spread the loveKUNA mambo machache mazuri ya kujifunza kutoka kwa Margaret Thatcher,...

error: Content is protected !!