Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari Sabaya kusuka ama kunyoa leo
HabariTangulizi

Sabaya kusuka ama kunyoa leo

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha nchini Tanzania leo Ijumaa tarehe 10 Juni 2022
Itatoa hukumu ya kesi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita. Aripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kesi hiyo ya uhujumu uchumi ilikuwa itolewe Jumanne ya tarehe 31 Mei 2022 lakini iliahirishwa kwa sababu Hakimu alyeisikiliza kesi hizo na kupaswa kutoa hukumu, Dk. Patricia Kisinda kuwa na majukumu mengine nje ya Jiji la Arusha.

Katika kesi hiyo, Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashitaka matano ya uhujumu uchumi, likiwamo la kuongoza genge la uhalifu, matumizi mabaya ya madaraka, kujihusisha na vitendo vya rushwa na utakasishaji fedha.

Mbali na Sabaya washitakiwa wengine katika shauri hilo ni, Sylvester Nyengu (26), Enock Togolani (41), Watson Mwahomange (27), John Odemba, Jackson Macha (29) na Nathan Msuya (31).

Katika kesi hiyo, Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashitaka matano yakiwamo ya uhujumu uchumi yanayokabili washitakiwa wote.

Ilidaiwa Sabaya akiwa mtumishi wa umma na wenzake, tarehe 20 Januari 2021 Arusha akiongoza genge la uhalifu katika maeneo mbali mbali ya mkoa huu na Kilimanjaro na akiwa Mkuu wa Wilaya, alitumia vibaya madaraka yake akijua wazi ni kosa kisheria.

Mashitaka ya pili dhidi yake Sabaya, ilidaiwa kuwa Januari 20 mwaka jana Arusha akiwa mtumishi wa umma, alishiriki kushawishi rushwa ya Sh milioni 90 kutoka kwa mfanyabiashara wa hapa, Francis Mrosso mkazi wa Kwa Mrombo.

Ilidaiwa kuwa alifanya hivyo ili amsadie katika kesi ya jinai ya ukwepaji kodi, iliyokuwa ikimkabili huku akijua wazi kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria, akiwa mtumishi wa umma.

Katika mashitaka ya tatu pia dhidi yake, ilidaiwa kuwa Januari 20 mwaka jana Arusha, aliomba rushwa ya Sh milioni 90 kwa Mrosso ili amsaidie katika kesi hiyo ya kodi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.

Kwenye mashitaka ya nne ya utakasishaji fedha dhidi ya washitakiwa wote saba, ilidaiwa kuwa Januari 20 mwaka jana Arusha, walipokea Sh milioni 90 za Mrosso na kwenda kuzifanyia matumizi haramu ambayo ni kinyume na sheria.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa huku Sabaya na wenzake wakiwa na kumbukumbu ya hivi karibuni kushinda rufaa katika hukumu nyingine iliyomfunga miaka 30 jela, hivyo adhabu yake kubatilishwa.

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilibatilisha hukumu ya miaka 30 jela na kuwaacha huru Sabaya na wenzake wawili, tarehe 6 Mei 2022.

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Sedekia Kisanya wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, aliyesikiliza shauri hilo la rufaa namba 129/2021 kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Jaji Kisanya alisema baada ya kupitia hoja za pande mbili, Mahakama imejiridhisha kuwapo upungufu wa kisheria kwenye mwenendo wa shauri hilo, hivyo akaamuru kuachwa huru kwa waleta rufaa hao.

Aidha, hukumu hiyo inatolewa huku Sabaya na wenzake wakiwa na kesi nyingine Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi Mkoani Kilimanjaro yenye mashtaka mbalimbali ikiwemo rushwa, utakatishaji fedha pamoja na kuongoza genge la uhalifu.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

error: Content is protected !!