Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Chongolo awapa ujumbe wa matumiani wakumila tumbaku
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo awapa ujumbe wa matumiani wakumila tumbaku

Katibu Mkuu CCM Daniel Chongolo katika moja ya ziara zake
Spread the love

 

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na maeneo mengine kuchangamkia kilimo cha tumbaku kwa kuwa tayari Serikali ya CCM imeshughulikia changamoto ya masoko. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga … (endelea).

Akizungumza katika ziara Wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Chongolo amesema ameagizwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwapa ujumbe wakulima wa mazao hayo kulima zaidi kwa kuwa kuna soko la uhakika la mazao hayo.

“Nimezungumza na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kuhusu mpango wa wakulima, ameniambia mpango ni kuzalisha tani laki moja au Kilogramu milioni 100 za mazao haya, maana yake ninyi wakulima muende kulima maeneo makubwa na kilimo kikubwa ili uzalishaji uanze kupanda kuanzia sasa”, amesema Chongolo.

Katibu Mkuu amesema mnunuzi mkubwa wa zao hilo la Tumbaku mkoani Morogoro, alikuwa na changamoto lakini hadi sasa changamoto hizo tayari zimetatuliwa na hivi karibuni Kiwanda hicho kitawashwa kwa ajili ya kufanya uzalishaji.

Amesema kiwanda hicho kinahitaji Kilogramu zaidi ya milioni 30 na zaidi hivyo wakulima hao wanapaswa kuchangamkia fursa kulima zaidi.

“Tumbaku inauzwa kwa Dola 1.65 ipo hapa inauzwa kwa madaraja ukiitunza vizuri zaidi inaenda hadi daraja la juu inauzwa Shilingi 5000 kwa kilo, sawa na Dola mbili na zaidi, zao la Pamba nalo limeni kwa kiwango kikubwa kwa sababu Soko lipo”, amesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

error: Content is protected !!