Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Chongolo atoa siku 60 kwa MSD kupeleka vifaatiba hospitali Ushetu
Habari Mchanganyiko

Chongolo atoa siku 60 kwa MSD kupeleka vifaatiba hospitali Ushetu

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo
Spread the love

 

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameitaka Serikali ichukue hatua za haraka na ndani ya miezi miwili ya Bohari ya Dawa (MSD) iwe imeleta vifaa tiba na vifungwe huduma za matibabu zianze kutolewa katika Hospitali ya Halmashauri ya Ushetu, Mkoa wa Shinyanga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga … (endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwasilishwa taarifa ya ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Ushetu iliyoanza kujengwa mwaka 2019 kwa gharama ya Sh.3.168 bilioni huku majengo yakikamilika lakini huduma inatolewa kwa jengo moja tu.

Akisoma taarifa hiyo leo Jumamosi, tarehe 28 Mei 2022 wilayani hapa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo, Dk Mbalu Maduhu mbele ya Chongolo alisema hiyo ni moja ya hospitali mpya 67 zinazoendelea kujengwa nchini lakini changamoto kubwa ni vifaatiba kutopelekwa hadi sasa.

Alisema hospitali hiyo ina majengo saba yote muhimu ya kutoa huduma kama vile jengo la wazazi, utawala, radiolojia, maabara, wodi magonjwa ya ndani, watoto, wodi ya upasuaji, jengo la kuhifadhi maiti na mengine na kwamba mengi ujenzi wake umekamilika ila vifaa tiba hakuna.

“Tuna upungufu wa vifaa tiba na rasilimali watu na hiyo imesababisha tuendelee kutoa huduma za Wagonjwa wa Nje (OPD) tu mpaka sasa,” alisema Dk Maduhu.

Naye Mbunge wa Ushetu (CCM), Emmanuel Cherehani alisema changamoto hizo alisema majengo mengi ya hospitali yamekamilika tangu mwaka 2020 lakini hayana vifaa tiba.

“Mheshimiwa katibu mkuu hospitali hii majengo mengi yamekamilika tangu mwaka 2020 lakini hayana vifaa tiba na hakuna huduma inayotolewa isipokuwa jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD), halmashauri ilishaipa MSD zaidi ya Sh.40 milioni ya vifaa tiba lakini hadi leo havijaletwa,” alisema Cherehani.

Alisema ujenzi wa hospitali hiyo umegharimu serikali fesha nyingi na hiyo yote
ni juhudi ya serikali kutatua changamoto ya kero ya umbali wa huduma za afya kwa wananchi.

Akizungumzia hoja hizo, Chongolo alisema ni lazima vifaa tiba viletwe ndani ya miezi miwili ijayo (siku 60) na kusema anawasiliana na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuhakikisha vifaa hivyo vinapelekwa haraka.

“Tumetembelea miradi ya maendeleo na hapa Ushetu tumetembelea mradi wa hospitali yenu ambayo tumeshuhudia jengo la OPD tu ndio linafanya kazi, mengine hayafanyi kwa sababu hakuna vifaa tiba, hii sio sawa maendeleo ni kuona majengo haya yanatoa huduma,” alisema Chongolo.

Aidha alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema kuwasiliana na Meneja wa MSD mkoani humo kuonana naye (Chongolo) ili aeleze sababu za kutopeleka vifaa tiba katika hospitali hiyo licha ya fedha za vifaatiba hivyo kupewa.

Vilevile Chongolo alisisitiza wananchi wa mkoa ya Shinyanga na maeneo mengine kuchangamkia kilimo Cha tumbaku kwa kuwa tayari serikali ya CCM imeshughulikia changamoto ya masoko.

2 Comments

  • Duh!
    Zile zingine 66 vipi?
    Ungetembelea zote ujionee na useme haya ningekuelewa. Lakini 1 kati ya 67 haitoshi. Tembea zaidi uone mengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!