Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mchina ahukumiwa miaka 20 jela kwa kuwachapa wafanyakazi viboko
Habari MchanganyikoTangulizi

Mchina ahukumiwa miaka 20 jela kwa kuwachapa wafanyakazi viboko

Spread the love

MAHAKAMA nchini Rwanda imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela raia wa China kwa mashtaka ya mateso aliyowafanyia wanaume wanne aliokuwa akiwachapa huku wakiwa wamefungwa kwenye mti. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hukumu hiyo iliyotolewa jana tarehe 20 Aprili, 2022 na Jaji Jacques Kanyarukiga, imekuja baada ya video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha Mchina huyo aliyefahamika kwa jina la Sun Shujun (43) akiwacharaza bakora wanaume hao mwaka jana.

Aidha, Renzaho Alexis ambaye ni raia wa Rwanda, naye amehukumiwa miaka 12 jela kwa kumsaidia Mchina huyo kuwaadhibu wanaume hao.

Waathiriwa hao ambao walikuwa wafanyakazi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya Ali Group Holdings Ltd inayosimamiwa na Shujun katika wilaya ya Rutsiro, walidaiwa kuhusishwa na wizi.

Akijitetea mbele ya Jaji huyo, Shujun alidai awali alikuwa amewaonya wezi baada ya mali zake kuibiwa mara kwa mara.

Pia alijitetea kuwa awali aliwalipa fidia waathiriwa wawili Dola za Marekani (1,338) Sh milioni 3.1 na kuwasainisha barua ya upatanisho.

Hata hivyo, upande wakili wa serikali alipinga utetezi huo na kudai kuwa waathiriwa hao walikubali fidia hiyo kwa kumuogopa Mchina huyo pamoja na kiwewe alichokuwa amewasababishia.

Mashahidi waliiambia mahakama kuwa Shujun alikuwa ameweka msalaba ambapo wale walioshukiwa kumuibia walifungwa na kuchapwa viboko.

Agosti mwaka 2021, video hiyo ya dakika tatu ilisambaa katika mitandao nchini Rwanda na kusababisha kukamatwa kwa Shujun – ambaye aliachiliwa kwa dhamana baadaye.

Video hiyo ilichukuliwa na wafanyakazi wenye hasira na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha, Ubalozi wa China mjini Kigali jana umetoa taarifa na kulaani vitendo visivyo halali kwenye video hiyo.

Pia ulitoa wito kwa raia wanaoishi nchini Rwanda, kuishi kwa kufuata sheria za nchi hiyo.

1 Comment

  • Grazie mahakama. Kwa kutimiza wajibu .mahakama za east somo ndio hilo ukezi sio kutesa watu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!