Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge ataka watu binafsi wapewe mikopo, vikundi vinakwama kurejesha
Habari za Siasa

Mbunge ataka watu binafsi wapewe mikopo, vikundi vinakwama kurejesha

Spread the love

MBUNGE wa Lupembe, Edwin Swale (CCM), ameishauri Serikali ifanye mabadiliko ya sheria yatakayowezesha asilimia 10 za mapato ya halmashauri zinazotolewa kwa ajili ya mikopo kwa wananchi, zitolewe kwa watu binafsi badala ya makundi maalumu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Akizungumza bungeni jijini Dodoma, leo Jumanne, Swale amesema utolewaji fedha hizo kwa ajili ya mikopo kwa watu binafsi itasaidia kurejeshwa katika halmashauri.

“Fedha nyingi za asilimia 10 hazirudishwi kwenye halmashauri zetu, ninayo aoni kwamba utaratibu huu wa kutoa fedha kwenye vikundi pengine hauwezi kuwa na ufanisi na nilikwua napendekeza wako wananchi binafsi wenye uwezo na mawazo ya biashara wanaweza kubuni mradi,”

“Badala ya kuendelea kutoa fedha kwenye vikundi vya watu watano hadi 10 tungeruhusu hizi fedha akopeshwe mtu mmoja,” amesema Swale.

Mbunge huyo wa Lupembe amesema, fedha hizo zikitolewa kama mkopo kwa mwananchi mmoja mmoja, zitazalishwa kwa ufanisi na kupelekea wananchi wengi kupata ajira kupitia miradi itakayoanzishwa.

“Ninaamini mtu mmoja mwenye wazo zuri la biashara anaweza kuajiri watu 100 kuliko watu kwenye vikundi, tunayo historia katika nchi hii, hizi biashara za watu wengi zimeshindikana huko nyuma. Biashara ya watu wengi ni ngumu kufuatilia,” amesema Swale na kuongeza:

“Ningependekeza tubadili sheria tuanze kutoa mikopo kwa mtu mmoja mmoja mwenye ujuzi au mradi mzuri, ili mradi ana sifa za kupewa mkopo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

error: Content is protected !!