Tuesday , 30 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa awatega ma-RC matumizi mashine za ukusanyaji mapato
Habari Mchanganyiko

Majaliwa awatega ma-RC matumizi mashine za ukusanyaji mapato

Spread the love

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa mikoa wahakikishe halmashauri zote nchini zinatumia vizuri mashine na mifumo iliyowekwa katika ukusanyaji wa mapato. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Aidha, Waziri Mkuu amewataka wakuu wa mikoa wasimamie suala la uadilifu kwenye ukusanyaji wa mapato.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo tarehe 14 Machi, 2022 wakati akizungumza na viongozi hao katika kikao alichokiendesha kwa njia ya video kutokea ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.

“Jiridhisheni kile kinachokusanywa na kiasi kinachopelekwa ni halisi. Lazima suala hili lisimamiwe kwa nguvu zote. Moja ya ajenda kubwa ni mapato, ukusanyaji wa mapato iwe ajenda namba moja katika ratiba zenu za utendaji kazi za kila siku,” amesema.

Amesema iwapo hawatosimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato bajeti zao hazitoongezeka na hivyo kuathiri utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amesema viongozi hao wanatakiwa wajiridhishe kama watendaji wa halmashauri wanamudu kufikia vyanzo vyote vya mapato, kuviratibu na kutumia mifumo sahihi ya ukusanyaji.

“Msiwaachie TAMISEMI pekee kusimamia ukusanyaji wa mapato, twende tukasimamie kwenye halmashauri zetu ili kuhakikisha makusanyo hayo yanaongezeka kila siku.”

Amewataka watendaji hao wahakikishe wanasimamia vizuri miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo yao na lazima ilingane na kiwango cha fedha kilichotolewa.

Pia, amewataka Watanzania wajivunie mafanikio yaliyopatika katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yapongezwa kuimarisha ubora na usahihi wa taarifa za Hali ya Hewa

Spread the love  WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

Habari Mchanganyiko

Bil 12.4 zimetumika ujenzi wa miradi wilaya ya Momba

Spread the love MKUU wa wilaya ya Momba mkoani Songwe Kennan Kihongosi...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

error: Content is protected !!