Saturday , 4 May 2024
Home Kitengo Michezo Nabi: Ni bahati kuwa na mchezaji kama Mayele
Michezo

Nabi: Ni bahati kuwa na mchezaji kama Mayele

Spread the love

 

KOCHA mkuu wa kikosi cha Yanga, Mohammed Nasredin Nabi hakusita kumwagia sifa mshambuliaji wake kiongozi, Fiston Mayele raia wa Jamhuri ya Congo mara baada ya kutupia kamabni mabao mawili, kwenye mchjezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa kwanza kwa duru la pili kwa Yanga, ulipigwa jana Jumapili Tarehe 27 Februari Mwaka huu, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari mara baada ya mchezo huo kukamilika, Nabi alifunguka kuwa Mayele ni mchezaji ambaye anajituma na mwenye mahusiano mazuri na wenzie na ni bahati kuwa na yeye.

“Mazoezini anawahi anajituma anamahusiano mazuri na wachezaji wenzie na viongozi, nampongeza kwa tabia hiyo ni bahati kuwa na mchezaji kama yule.” Alisema Nabi

Kwenye mchezo huo dhidi ya Kagera Sugar, Mayele alipachika mabao mawili kwenye dakika za 30, 50 na kufikisha idadi ya mabao 9 kwenye msimamo wa wafungaji akishika nafasi ya pili nyuma ya mshambuliaji wa Namungo FC, Relient Lusajo.

Aidha kwa upande mwengine Nabi alisifu nidhamu anayoonyesha mchezaji huyo, licha na umaarufu alioupata nchini Tanzania ndani ya muda mfupi.

“Kuhusu Mayele siwezi kuzungumzia kuhusu magoli, lakini ni mchezaji mwenye nidhamu pamoja na umaarufu wote aliyopata.”

Ikumbukwe Mayele alijiunga na Yanga kwenye dirisha kubwa la usajili  mwezi Agosti, akitokea klabu ya AS Vita inayoshiriki ligi Kuu nchini Congo na kwenye msimu uliomalizika alishika nafasi ya pili kwa kupachika mabao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

error: Content is protected !!