Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Michezo Kapombe, Inonga, Banda kuchuana
Michezo

Kapombe, Inonga, Banda kuchuana

Spread the love

 

MABEKI wa klabu ya Simba Shomary Kapombe na Henock Inonga sambamba na kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Peter Banda wamewekwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki wa klabu hiyo kwa mwezi Februari. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Tuzo hiyo ya mashabiki (Emirates Aluminium ACP Simba Fans) hutolewa kila mwezi kwa mchezaji ambaye amefanya vizuri kwenye michezo husika.

Kwa upande wa Kapombe ameingia kwenye tatu bora mara baada ya kucheza michezo minne ndani ya mwezi Februari, huku akifunga bao moja na kuhusika katika mabao mengine manne.

Peter Banda ndani ya mwezi huo huo alicheza michezo minne, na kufunga bao mmoja kama ilivyo kwa Kapombe na kuhusika katika mabao manne mengine yaliyofungwa kwenye michezo hiyo.

Aidha kwa upande wa beki kisiki wa klabu hiyo Ingona yeye amekuwa na msimu mzuri toka alipojiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye dirisha kubwa la usajili na kucheza michezo mingi ulilinganisha na baadhi ya wachezaji waliosajili kwa msimu huu.

Inonga katika mwezi Februari amecheza michezo zote sita za mwezi Februari akiwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Ikumbukwe mshindi wa tuzo hiyo atakabidhiwa kiasi cha Shilingi 2,000,000 na wadhamini wa tuzo hiyo, kampuni ya Emirates Aluminium ACP.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

error: Content is protected !!