May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Pinda ataka mjadala mchango wa Mwalimu Nyerere maendeleo ya Tanzania

Mizengo Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mizengo Pinda, ameshauri liundwe jukwaa la kujadili mchango wa mwasisi huyo katika utatuzi wa matatizo yaliyoikabili Tanzania. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Pinda ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, ametoa wito huo hivi karibuni, katika kikao cha kawaida cha Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Aliwataka viongozi wa sekretarieti ya taasisi hiyo, kuendeleza fikra, falsafa pamoja na kuyaishi mawazo ya Mwalimu Nyerere.

Pinda alitoa wito kwa wajumbe hao kutekeleza majukumu yao pasina kuegemea kwenye masuala ya udini, ukabila na siasa, bali wajike katika malengo ya uanzishwaji wake pamoja na kuzingatia katiba, kanuni na miongozo iliyowekwa kisheria kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Aidha, Pinda amesema yupo tayari kufanya kazi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya taasisi hiyo, kwa kusimama kidete katika kufanikisha mambo mbalimbali, ikiwemo maadhimisho kuelekea miaka 100 ya kumbukizi ya kuzaliwa, Mwalimu Nyerere.

“Nafarijika sana kuona kwamba watu wanaelewa nini nchi hii inahitaji, sasa ni jukumu la kusukuma wazo hili. Sasa kuna dalili kwamba tunaweza pata jukwaa la kuzungumza wapi tulipo, nini kilichotokea wakati ule na ni namna vipi tulifanikiwa kutatua matatizo ya wakati ule,” alisema Pinda na kuongeza:

“Ukiuliza nani alikuwa nyuma ya ushawishi wa aina hii wanasema Mwalimu Nyerere, haitoshi kujua jina la Mwalimu Nyerere, ni vizuri kumjua ndiyo tuweze kuhubiri haya mambo vizuri sana.”

Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Paul Petro Kimiti, amesema wameanzisha kanda maalumu kama sehemu ya mikakati ya kuhakikisha wanamuenzi Mwalimu Nyerere.

Kikao hicho kililenga kujadili uimarishwaji wa shughuli za taasisi hiyo, ikiwemo za kusaidia wananchi, makundi ya watu mbalimbali, vyama vya siasa, taasisi binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Katika kuhakikisha amani,utulivu, mshikamano vinadumu pamoja na kukabiliana na maadui watatu, maradhi, ujinga na umaskini huku suala la rushwa likiwekewa msisitizo mkubwa kwa kuishauri Serikali namna ya kuyitokomeza.

Kikao hicho kilihudhuriwa na watu mbalimbali mashughuli, ikiwemo John Shibuda na wajumbe wa bodi hiyop, Zakhia Meghji na Maua Daftari.

error: Content is protected !!