Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa NATO yaonya Urusi kushambulia Ukraine
Kimataifa

NATO yaonya Urusi kushambulia Ukraine

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Jens Stoltenberg amesema Urusi imepanga kufanya mashambulizi dhidi ya Ukraine. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza katika kongamano la usalama mjini Munich nchini Ujerumani, Stoltenberg, ameliambia shirika moja la utangazaji la Ujerumani kwamba hatari ya shambulio iko juu.

Mashariki mwa Ukraine, mapigano mapya yamezuka katika muda wa wiki moja iliyopita kati ya serikali ya Ukraine na vikosi vinavyotaka kujitenga vinavyoungwa mkono na Urusi.

Takriban visa 2,000 vya ukiukaji wa mapatano ya kusitisha mapigano vilirekodiwa na waangalizi wa Ulaya katika eneo hilo siku ya Jumamosi.

Washirika wa Magharibi wa Ukraine wana wasiwasi kwamba Urusi imejiweka tayari kufanya mashambulio ya kijeshi dhidi ya Ukraine.

Hata hivyo Urusi imekanusha mipango yoyote ya kushambulia taifa hilo jirani.

Wanajeshi wawili wa Ukraine wameuawa na wanne kujeruhiwa kwa makombora siku ya Jumamosi ikiwa ni vifo vya kwanza kuripotiwa katika wiki kadhaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!