Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shahidi: Mbowe alikuwa na nia ovu, hakumtafuta mlinzi wake Polisi
Habari za SiasaTangulizi

Shahidi: Mbowe alikuwa na nia ovu, hakumtafuta mlinzi wake Polisi

Spread the love

 

MPELELEZI wa kesi ya uhujumu uchumi namba 16/2021, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, Inspekta Tumaini Swila, amedai mwanasiasa huyo alikuwa na nia ovu ndiyo maana hakumtafuta mlinzi wake, Halfan Bwire Hassan, alipokamatwa na Jeshi la Polisi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Inspekta Swila ametoa madai hayo, leo Jumanne, tarehe 15 Februari 2022, katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, jijini Dar es Salaam, akisoma maelezo yake ya ushahidi, anayodaiwa kuyaandika tarehe 6 Agosti 2021.

Mbali na Mbowe na Hassan, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya, ambao wanakabiliwa na mashtaka sita ya ugaidi, ikiwemo kupanga njama za kudhuru viongozi wa Serikali.

Mkaguzi huyo Polisi, kupitia maelezo yake hayo amedai, licha ya kwamba Hassan alikuwa mlinzi wa karibu wa Mbowe, mwanasiasa huyo hakumtafuta katika vituo vya polisi kujua tatizo ni nini.

Amedai kwa mujibu wa upelelezi wake, mazingira hayo yanaonesha Mbowe na wenzake, walikuwa na nia ovu.

Mahojiano kati ya Wakili wa utetezi, Peter Kibatala na Inspekta Swila yalikuwa kama ifuatavyo;

Kibatala: Nilikuuliza iwapo ni kweli katika maelezo yako kuna maneno, lakini tangu mukamatwa kwa Bwire ukaenda mpaka pale nia ovu, umeona hilo eneo?

Shahidi: Nimeona.

Kibatala: Hiyo sehemu ni moja wapo ya conclusion (hitimisho) iliyokuonesha lazima ana nia ovu ya makosa ya kigaidi? Kwamba angekuwa na nia safi angekuja kituoni kumtafuta, ndiyo ulitaka kutuaminisha hivyo?

Shahidi: Ndiyo kuonesha conduct yake.

Kibatala: Sheria gani inalazimisha hivyo?

Shahidi: Katika hatua zangu za kipelelezi.

Kibatala: Ni sheria gani ina mlazimisha Mbowe amtafute Bwire personal?

Shahidi: Hakuna.

Kibatala: Katika ushahidi wako wote ulimwambia Jaji ni ndugu yake yupi au jamaa yake yupi, mliyeruhusu Bwire amtaarifu mimi Bwire mume wako au mwajiriwa wako niko kituo fulani. Ili kuwezesha wengine kwenda kumtafuta, ulimwambia Jaji kuhusu hilo eneo?

Shahidi: Rudia.

Kibatala: Ili Mbowe aende kumtafuta Bwire lazima awe na taarifa, swali langu katika ushahidi wako kuna mahali ulimwambia Jaji tulimpa ‘facility’ Bwire kuongea na ndugu au mwajiri wake kumfahamisha mimi Bwire nimekamatwa?

Shahidi: Sikueleza, ilikuwa inafahamika wapi yupo mtuhumiwa.

Kibatala: Hiyo unaposema ilkuwa inafahamika, inafahamika na nani?

Shahidi: Alienda kupekuliwa kwake baada ya kuficha haishi Dar es Salaam, anaishi Ngerengere. Ikafahamika ukafanyika upekuzi alikuwa mke wake.

Kibatala: Ilikuwa inafahamika kwa Mbowe?

Shahidi: Ilikuwa inafahamika na mke wake.

Kibatala: Katika upelelezi wako uligundua mke wa mshtakiwa ana mawasiliano na Mbowe, ulichunguza?

Shahidi: Sikujithibitishia

Kibatala: Unafahamu mara baada ya wenzake kufikishwa mahakamwni Mbowe alituma mawakili wali-apear mara kadhaa kumuwakilisha Bwire, unafahamu hilo?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Mbowe alielekeza mawakili waende kulinda maslahi ya kisheria ya Bwire, anakuwa haja-participate kwenye walfare ya mwajiriwa wake?

Yaani Mbowe badala ya yeye yuko busy na mambo ya uchaguzi akatoa hela, akampa Wakili Mndeme nenda mahakamani?

Shahidi: Nilichokuwa naongelea kwenye maelezo yangu, tangu amekamatwa tarehe 9 Agosti 2020 na tarehe 10 Agosti 2020 akapekuliwa, mpaka tarehe 19 Agosti 2020 anafikishwa mahakamani, hajamtafuta katika Kituo cha Polisi.

Kibatala: Nasema wewe katika investigation conlusion zako ni kwamba, Mbowe ana nia ovu ndiyo maana hakuwatafuta wenzake.

Kama kweli alituma na committal ikionesha wakili amekwenda mahakamani kwa maelekezo ya Mbowe, atakuwa haja-participate?

Shahidi: Nitajuaje kama alituma wakati nimekwambia sijui kama alituma mahakamani.

Inspekta Swila anaendelea kuulizwa maswali na Wakili Kibatala.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!