Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba: Nafasi yangu iko wazi 
Habari za Siasa

Prof. Lipumba: Nafasi yangu iko wazi 

Prof. Ibrahim Lipumba
Spread the love

 

MWENYEKITI  wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa. Ibrahim Lipumba, amesema nafasi yake iko wazi kwa yeyote atakayetaka kugombea kwenye uchaguzi wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Prof. Lipumba ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, tarehe 12 Februari 2022, akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

“Natoa wito na kuwahakikishia wanachama kwamba, hii nafasi ya mwenyekiti iko wazi kwenye uchaguzi unaokuja, kwa maana kwamba kila mmoja anaweza kugombea nafasi hiyo,” amesema Prof. Lipumba.

Mwenyekiti huyo wa CUF, amesema lengo la kutoa kauli hiyo ni kuonesha kuwa hajawahi kuwa kikwazo kwa watu kugombea nafasi hiyo na kwamba kila mwanachama wa chama hicho anayo nafasi ya kugombea nafasi za juu za uongozi.

“Nasisitiza vijana wajitokeze kugombea nafasi zote ikiwa ni pamoja na nafasi ya mwenyekiti wa Taifa, kwamba Lipumba hajawa na hatokuwa kikwazo kwa watu kujitokeza kugombea nafasi hizo,” amesema – Prof.  Lipumba.

Aidha, Prof. Lipumba amesema anahitaji apate muda wa kukamilisha machapisho yake kuhusu ushiriki wake kwenye mapambano ya kudai haki, demokrasia na maendeleo ya uchumi wa Watanzania.

“Binafsi umri umekwenda Mingu akinijalia najitaji nipate muda wa kukamilisha machapisho ya ushiriki wangu katika mapambano ya kudai haki kwenye mapambano ya demokrasia na maendeleo ya uchumi wa Tanzania, wajibu wangu kuhakikisha chama kinakuwa imara na kupambana ili nchi yetu ipate haki,” amesema Prof. Lipumba.

Aidha, Prof. Lipumba amewaomba Watanzania waongeze ushiriki wao katika siasa ili wajenge demokrasia na vyama vya siasa vilivyo imara.

1 Comment

  • TZ TUNA MAHASIDI WA DEMOKRASIA HAWA (2) “LIPIMBA” NA “MREMA” HAO NDIO VIKWAZO VYA KUFIKI MALENGO YETU KAMA TAIFA TUKIWAACHA HAO VIPAKA SHUME HAMAD RASHI NA JOHN CHEYO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!