Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Ummy akabidhi taulo za kike kampeni ya ‘Binti Ng’ara’
Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy akabidhi taulo za kike kampeni ya ‘Binti Ng’ara’

Spread the love

 

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa msaada wa taulo za kike paketi 1000 kwa Shirika lisilo la Kiserikali la Victoria Foundation kwa watoto wa kike waliopo shuleni, ambao hukumbwa na changamoto ya kushindwa kuhudhuria masomo kipindi cha hedhi jambo ambalo linalowarudisha nyuma kitaaluma. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Akikabidhi msaada huo kwa Mkurugenzi wa Shirika hilo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya zilizopo jijini Dar es salaam leo tarehe 12 Februari, 2022, Ummy amesema amepata msukumo wa kutoa taulo hizo ili kuunga mkono kampeni ya “Binti Ng’ara, Timiza Malengo” inayotekelezwa na Victoria Foundation kwa ajili ya kuwasaidia mabinti wanaokosa uwezo wa kununua taulo hizo.

Waziri Ummy amesema kampeni ya Binti Ng’ara ni kampeni nzuri kwani imelenga kumuinua mtoto wa kike ambaye alikuwa anakosa taulo inayomwezesha kujistiri pindi anapokuwa kwenye siku zake.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Victoria Foundation, Vicky Kamata ameshukuru kwa msaada huo kutoka kwa Waziri Ummy na kusema utakuwa msaada mkubwa kwa watoto wa kike ambao wamekuwa wakishindwa kuhudhuria masomo yao kutokana na kuwa kwenye hedhi na hivyo kusubiri mpaka wamalize ndiyo waendelee na masomo.

Kamata ametoa ombi kwa wadau wengine kujitokeza katika kuchangia kampeni hiyo, ili kuweza kuwasaidia mabinti hao wanaokosa masomo pindi wanapokuwa kwenye hedhi, na kuweza kuwasaidia kuondokana na changamoto hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!