Saturday , 4 May 2024
Home Kitengo Michezo 10 wa kwanza kuchanja kuiona Simba, Mtibwa buree!
Michezo

10 wa kwanza kuchanja kuiona Simba, Mtibwa buree!

Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru
Spread the love

 

WAKATI homa ya mtanange unaotarajiwa kupigwa kesho tarehe 22 Januari, 2022 kati ya Simba SC. na Mtibwa Sugar, mashabiki wa timu hizo wameshauriwa kupata chanjo ya UVIKO-19 kujishindia tiketi bure. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Wito huo umetolewa na Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru katika uwanja wa Manungu, Turiani mkoa Morogoro.

Kifaru amesema watu 10 wa kwanza kupata chanjo hizo watajishindia tiketi za kuushuhudia mchezo huo bure.

“Kwa kutambua umuhimu wa chanjo mimi nitakuwa mtu wa kwanza kupata chanjo, hivyo niwaombe na wananchi kupata chanjo kwa kuwa ina umuhimu mkubwa,” amesema Kifaru.

Shaaban Kado

Aidha, Kifaru amesema baada ya kupata elimu juu ya UVIKO-19 ndipo alipofanya maamuzi ya kupata chanjo ili kujikinga mwenyewe na kukinga watu wake wa karibu.

Hata hivyo, Mtendaji Mkuu wa Timu ya Mtibwa Sugar, Swabri Aboubakar amesema hii ni fursa kwa mashabiki 10 wa kwanza kupata huduma ya chanjo kupatiwa tiketi za kuingia kutazama mchezo huo.

“Kwa kutambua juhudi za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan na sisi kama viongozi tunawasihi wachezaji wetu na mashabiki wetu kupata chanjo ya UVIKO-19 ili tucheze kwa Furaha na kujiamini,” amesema Swabri.

Abdi Banda

Wakati mlinzi wa timu hiyo, Abdi Banda amesema alishapata chanjo baada ya kujua umuhimu wake ili ailinde familia yake.

“Mimi nimechanja kwa kujua umuhimu wake na wewe kachanje ili ujikinge mwenyewe na uwakinge wa karibu yako,” amesema Banda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

error: Content is protected !!