Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Washindi 100 wa NMB MastaBata wanyakua milioni 10
Habari Mchanganyiko

Washindi 100 wa NMB MastaBata wanyakua milioni 10

Spread the love

 

WATEJA 100 wa kwanza wa kampeni ya NMB MastaBata-Kivyako Vyako wamepatikana na kujinyakulia Sh.100,000 kila mmoja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Promosheni ya MastaBata Kivyako Vyako ilizinduliwarasmi katikati ya Disemba 2021 kwa lengola kuchagiza matumizi ya kadi za malipo za Mastercard kama sehemu ya mchango wa benki hiyo katika juhudi za taifa za kujenga uchumi usiotegemea fedha taslimu.

NMB pia inatumia kampeni hiyo kuendeleza uchumi wa kidijitali kurudisha fadhila kwa wateja wake waaminifu ambao wamekuwa ni muhimu wa safari yake ya mabadiliko ya kidijitali.

Akizungumza wakati wa droo ya kuwapata washindi wa kwanza wa MastaBata-Kivyako Vyako, jana Alhamisi, tarehe 6 Januari 2022, Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi wa NMB, Ali Ngingite, alisema zaidi ya Sh.200 milioni zitanyakuliwa kwenye kampeni hiyo ya miezi mitatu.

“Hili ni toleo la tatu la kampeni za MastaBata zilizoanza rasmi mwaka 2018 kuwahamasisha wateja na wasiowateja wa Benki ya NMB kutumia kadi za Mastercard wanapofanya malipo na miamala kupitia intaneti,” alisema Ngingite

“Kama watangulizi wake, promosheni ya MastaBata-Kivyako Vyako pia ina lengo la kuwatambua na kuwazawadia wateja wetu waaminifu kwa kuendelea kutumia huduma zetu,” alisema Ngingite

Wakati washindi 100 wa kila wiki watashinda Sh.100,000 kila mmoja, 25 watanyakua Sh.1 milioni kila mwezi na 30 wa mwisho watashinda jumla ya Sh.90 milioni zikiwa ni Sh.3 milioni kwa kila mshindi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!